Wa Ba-Werrasonique Kuja Hapa! Karibu Werrason Igweee !

Wa Ba-Werrasonique Kuja Hapa! Karibu Werrason Igweee !

MPUNGA

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2010
Posts
838
Reaction score
561
Nimeamua kwa ufupi kwa wapenzi wa muziki wa Congo na haswaa wale wa Werrason au wenye Werrasonique tuje hapa tujikumbushe machache ya nguli huyu ambaye wiki tumepata bahati ya kupatiwa ile adimu murua tuliyokosa kwa muda mureefu sana na kulishwa matango pori ya hawa wa hapa hapa.

VIBAO VYAKE WAKATI WA WENGE YA ZAMANI WENGE MUSICA BCBG


KASKIN Hii ni moja ya nyimbo za kwakwe Le Roy De La Forret Ngiama Makanda Igweeee ambayo ilipigiwa kura kuwa ni utunzi bora wa vijana wa Wenge Musica ambacho kipindi hicho walikuwa wanafanya muziki kama ni burudani tu wakitoka vyuoni. Ambapo wakati huo walikuwepo waanzilishi watano aliyebuni jina la wenge mpiga Bass Guitar Didier Masela, Noel Ngiama Makanda “Le Roy De La Forret Le Phenomena”, Allain Makaba mpiga Solo balaaa kuwahi kutokea, Aime Bwanga ambaye baadaye alijitoa na kuanzisha Wenge Aile Paris, na Blaise Bulla “ “ingineur” au “engineer” kwa kiingereza baadaye wakakaribishwa JB Mpiana ambaye alikuja kupewa heshima ya kiongozi wa bendi pamoja na Werrason kutokana na kipaji chake cha kuimba na Adolphe Domininguez mtoto wa tajiri maarufu aliyekuwa akiwasaidia mavazi na kifedha lakini shughuli yake kwenye steji ilikuwa ni balaa




Surprise Kapangala

Katika huu wimbo huyo Igweee Le Roy De La Forret alionesha umahiri mkubwa wa kunata na beats



Kibao kingine cha kunata na beat cha Werrason Tchacho Mbala ni balaaaaa!



Kalay Boeing

Huu ndiyo utunzi wake Werrason ambao uliipaisha na Wenge Musica BCBG kwenye anga za kimataifa na kuvunja kuvunja kabisa nguvu ya Soukouss ambayo uchezaji wake ulikuwa wa nguvu nyingi usiokuwa na staha na madaha



Remix yake baada ya kutengana na JB Mpiana na kuanzisha kundi lake la Wenge Maison Mere ( Makao Makuu ya Wenge) Hapa alikuwa na manguli kama akina Ferre Gola, Adolph Dominguez “Papa Tonya Tonya” , Baby Ndombe, La Coste



Kalay Boeing live na vijana wake wa Wenge Maison Mere – Zenith 2008



WERRASON NA BENDI YAKE WA WENGE MUSICA MAISON MERE (WMMM) MAKAO MAKUU YA WENGE

Vibao vilivyompatia umaarufu baada ya kutengana na JB Mpiana

SOLOLA BIEN (Zungumza vizuri ambalo lilikuwa ni dongo kwa hasimu wake kipindi hicho JB Mpiana ambaye alikuwa rafiki yake kipenzi ) ambacho kilimpatia taji la GOLDEN DISK UFARANSA baada ya mauzo yake kuvunja rekodi ya zaidi ya nakala 300,000 kuuzwa UFARANSA na kujipatia Tuzo ya Kora Award. Hapa alivunja vunja kabisa uchezaji wa ndombolo na kuja MGHANI MPYA au “ATALAKU” au “RAPPER” aliyejulikana kama BILL CLINTON akija na ghani mpya ambazo zimebamba mpaka kizazi hiki cha leo.



Ndani ya Solola Bien kuna kibao matata cha rhumba alichoimba FERE GOLA cha VITA IMANA



Nyota ya Werrason ikaendelea kungaa baada ya kuja na mitindo ya KOYIMBI KOOO ambayo hapa illiigwa kipindi Fulani na msanii mmoja aliyejipatia umaarufu Afrika Mashariki ambaye baadaye maisha yake yalikuja kuporomoka sana hata kushindwa kupata vijisenti vya kujikimu.



Baada ya hapo ikafuata show kabambe ya ZENITH 2001 AMBAYO haijawi kuvunjwa rekodi mpaka leo na mwanamuziki yeyote toka Afrika hii ilikuwa ni DOUBLE ZENITH



Hakuna mapinduzi makubwa aliyoleta Werrason kama kachumbari za Werrason ambazo ziliigwa na bendi kadhaa ikiwemo kama za kwetu mnakumbuka kipindi cha akina marehemu Aisha Madinda, Lilian Internet Twanga PEPETA, zile zilikuwa ni carbon copy za Werrason



Koffi Olomide alisifiwa kwa Kisanola lakini Kisanola ni yak wake Werrason ambapo walikuwa wanamuimba Bill Clinton baada ya kutimka kwa Werrason kwamba achukue chanuo achane nywele zake maana jamaa alikuwa anasuka rasta. Hapa maatalaku walikuwa nu Yule Roi David “Mbilikimo” na CELEO SCRAM



Kachumbari za Werrason wengine walijitia kutudanganya kuwa wamekuja na style mpya ya “Bomoa Bomoa”, wengine wakatuimbia cheza “mgongo mgongo” lakini madini yalikuwa yanatoka hapa



Leeee leeeeee leeeeeeee Noel Ngiama analeta mambo nafikiri wengi mtakuwa mmeisikia hapa. Kuna kijana mmoja wa Bongo Flava alisema kabisa jina la Werrason mwishoni mwa wimbo wake wa “Malewa”



Werrason ana mengi sana ! Live yake ni ya Ukweeee! Ameleta mageuzi makubwa sana ya muziki wa Congo. Ni Kiongozi wa ubunifu wengine hufuatia. Vijana wasanii waje wajifunze Live Show zinavyopigwa siyo kutulisha matango pori hapo tarehe 6 April 2018. Nisiwachoshe maana siwezi kumaliza yote ya NOEL NGIAMA LE ROY DE LA FORRET (MFALME WA MISITUNI) mwenye MKANDA MWEUSI WA JUDO NA BALOZI WA AMANI WA UNICEF

Tumalizie kidogo KOFFI AYINA –

 
Sema kiingilio itakuwa shiling ngapi watu tukate ticket za fastjet fasta hapa. Tuje tumune Sarah solo, mdada ni hatari kuliko shetani kwenye gita huyu.
 
Sema kiingilio itakuwa shiling ngapi watu tukate ticket za fastjet fasta hapa. Tuje tumune Sarah solo, mdada ni hatari kuliko shetani kwenye gita huyu.
Akikujibu na mimi unitag mkuu,sio ya kukos hii.
 
Kiongozi jina la jamaa alie imba verse kabla ya Werasson hajamalizia kwenye kalay boeing ni nani ambae verse hiyo kwenye remix kaiimba Ferre Gola?
 
Back
Top Bottom