Vyura muhimu kuliko maendeleo ya mkoa kigoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vyura muhimu kuliko maendeleo ya mkoa kigoma

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Milindi, Jun 17, 2010.

 1. M

  Milindi JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2010
  Joined: Mar 3, 2009
  Messages: 1,214
  Likes Received: 375
  Trophy Points: 180
  Mpaka sasa siamini kweli ati vyura wamesababisha ujenzi wa mtambo wa kufua umeme mto malagalasi mkoani Kigoma kufutiliwa mbali na hawa wamarekani,Kitu cha kujiuliza hivi tunapata faida gani kwa kuwa na hawa vyura(wanyama hai..???).Watalii wangapi wametembelea eneo hilo na pesa kiasi gani mkoa wa kigoma umepata kutokana na kuwa na hao wanyama hai.JK kwa kumuogopa Zitto Kabwe Kajenga barabara kuunganisha kata za Jimboni kwa Zitto kama ile ya kuunganisha Chalinze na bagamayo.Vilevile daraja katika mto malagalasi mpaka leo ni kitendawili.Pamoja na mradi huo wa umeme kusemekana kuwa inatafutwa eneo jingine nafikiri itachukua mingi maana ahadi ya kujenga chanzo cha umeme ni zaidi ya mika ishirini iliyopita.Na kama hao wanyama hai kweli wana faida kwa mkoa kwa nini wasihamishiwe eneo jingine kwani mto malagalasi ni mrefu na eneo hilo ambalo ni zuri kwa ujenzi wa bwawa hilo la kufua umeme ujenzi ukaendelea.Mpango wa kutafuta eneo jingine ni upotezaji wa muda.Wabunge wa CCM jifunzeni kutoka kwa Mheshimiwa Zitto kabwe kwani amelitetea jimbo lake na limepata barabara ya lami wakati barabara kongwe Kigoma mpaka Nyakanazi(Bukoba) ikiwa katika hali ilelei wakati ndio barabara kuu ya kuunganisha mkoa.Ni vizuri wabunge wa kasulu na kibondo mkaungana na kuondoa shilingi ili barabara hii ipate kutengenezwa kwa kiwango cha rami .Zitto anatafuta habari nyingi na siri nyingi za serikali anazo mpaka JK mwenyewe anagwaya asipojengewa barabara akatoa vitu hivyo hadharani basi inchi inaweza kuchafuka ndio maana wamempoza kwa kujenga barabara jimboni mwake.MwISHO KABISA HAO WANYAMA HAI WAHAMISHWE NA KITUO CHA UMEME KIJENGWE ILI KIGOMA NAYO IPATE MAENDELEO.Hizo Generator alizozindua JK subirini baada ya uchaguzi itakuwa giza na wana mageuzi wa Kigoma wembe uleule mapaka mafisadi wote waondoke madarakani.Mhesimiwa Zitto baada ya kupata barabara ya lami jmboni mwako sasa kilichobaki ni kuhakikisha kuwa daraja la mto malagalasi linajengwa,maana mpaka sasa huruma ya wakorea kujenga daraja hilo hatujui kinachoendelea natumaini kigoma kuna mtandao na mheshimiwa zitto utaisoma hii na kutupatia hali halisi baada ya kummwagia misifa JK natumaini na daraja utaweza kumshauri ili likamilike kabla ya uchaguzi.
   
Loading...