Vyuo vyote vigome ila sio Mzumbe

Vyuo vyote vigome ila sio Mzumbe

Wissman

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2014
Posts
1,034
Reaction score
1,319
Katika hali ya kushangaza migomo mbalimbali huwa inaendeshwa na wanafunzi wa vyuo mbalimbali hapa nchini (kama ilivyo sasa) lakini kwa hali ya ajabu na kustaajabisha kwa miaka mingi hapajakuwa na mgomo wa wanafunzi wa chuo kikuu Mzumbe. Nini siri ya wasomi wa chuo hicho? Wanawezaje kukabiliana na changamoto ambazo wasomi wa vyuo vikuu vingine Tanzania wameshindwa kuvumilia? Wao wanawezaje kujikimu kama fedha hazijafika kwa vyuo vyote? Kama wana mbinu ni ipi? Ili vyuo vingine navyo viige?
 
Mazingira ya maisha ya Mzumbe hayana changamoto nyingi ukilinganisha na mwanafunzi anayesoma IFM au UDSM, au CBE ya Dar. Kwa hiyo shida nadhani zipo ila zinavumilika. Miaka ya nyuma hakukuwa na migomo kwa sababu wanafunzi wengi walikuwa private!
 
Kuna wakati chuo hukopesha wanafunzi kiasi Fulani cha pesa halafu hela za bodi zikifika wanakata deni lao hivyo haiwapi sababu ya kugoma (talking from experience)
 
Mzumbe kuanzia uongozi mpaka waalimu kiukweli wapo well organized. Kwa hilo nawasifu. Hakunaga njaanjaa za hovyo. Pia Jumuiya ya Mzumbe wanajiheshimu sana. Hakuna utoto toto too much. Vyuo vingine vijifunze pale. Ila sisemi ndio serikali iwe inachelewesha pesa za wanafunzi..la hasha! Haki na stahili za wanafunzi ziwe zinapelekwa kwa wakati.
 
Mzumbe kuanzia uongozi mpaka waalimu kiukweli wapo well organized. Kwa hilo nawasifu. Hakunaga njaanjaa za hovyo. Pia Jumuiya ya Mzumbe wanajiheshimu sana. Hakuna utoto toto too much. Vyuo vingine vijifunze pale. Ila sisemi ndio serikali iwe inachelewesha pesa za wanafunzi..la hasha! Haki na stahili za wanafunzi ziwe zinapelekwa kwa wakati.

Kujifunza hayo unayosema ni kufundisha wanafunzi wawe km mbwa koko wasidai haki zao. Badala ya kuziamuru mamlaka husika kuwa well organized na kutekeleza majukumu yao ww unasema Mzumbe wapo well organized sio kweli
 
Lakini kitu cha kuongezea hawa vijana wetu wakumbuke tu kuwa huo ni mkopo, baadae watahitajika kurudisha hizo fedha wanazopewa sasa hivi.
 
Mzumbe wana uongozi makini unaojali matatizo ya Wanafunzi huwezi kusikia migomo ya kijinga Boom likichelewa chuo kinawakopesha.
 

Attachments

  • 1432151710300.jpg
    1432151710300.jpg
    31.8 KB · Views: 195
  • 1432151732011.jpg
    1432151732011.jpg
    57.5 KB · Views: 179
Wazeee wapo weng pale wanajiendeleza wanawasapot vijana ambao ni direct
 
Back
Top Bottom