Ndugu Mallaba, una hoja nzuri sana hasa kwa wanaoanzisha vyuo bila mpangilio. Nikukumbushe kuwa UDSM haikuanza kama Chuo kikuu bali kama college of East Africa University. Hii EA Univesity ilianza kwa kuwa Clollege of London University(kama nipo sahihi kwa London).
SUA haikuanza kama SUA bali UDSM Faculty then College of Agriculture. Muhimbili ilikuwa College of UDSM hadi hivi karibuni.
KCMC ina affiliation na Chuo Kikuu kimoja maarufu cha Ujerumani. Ili Chuo kipate hadhi ya kutambuliwa kuna mambo kama Research, Professors, Students, Facilities vinaangaliwa. UDSM inajulikana Duniani kwa kupitia watu kama kina Nyerere (Mkuu wa Chuo), Walter Rodney, na maelfu ya Wataalamu waliopita hapo. Kina Exchange program na Vyuo vingi tu. Hata kama bado hakijafikia ubora wa vyuo kama Witsrand kule Bondeni lakini ni ukweli kuwa kinajulikana. Unapoanzisha Chuo bila kuwa na back up ya Chuo maarufu itachukua miaka mingi sana kutambuliwa.
Soma attachment yako, utaona WHO wame address Muhimbili Health College, halafu wakasema Institute of Health Research. Ukweli ni kuwa Health research ni Institute kama Faculty pengine, lakini WHO inapata mchango mkubwa wa kitaalamu kutoka Institute hiyo ndio maana wana Recognized.
Si Vyuo vya Afya tu hata Vinginevyo. Utashangaa kuwa Chuo cha ushirika moshi ambacho ni tawi la SUA kitapata recognition haraka kuliko Josia Kibira, Tumaini, Morogoro Islamic, Bugando au Tumaini.
Ni rahisi sana kuita Chuo Kikuu, lakini ni ngumu sana kuwa recognized University.
I have a lot of interest on this issue. Is there anything that stakeholders can do to make sure that some of these schools are recognized by WHO?
Count me in if there is anything that needs to be done by stakeholders.
Mallaba
shukrani kwa Observation
Kimsingi Tanzania kuna uzembe wa hali ya juu kila idara ya serekali hususani kwenye hizi taasisi za elimu ya juu,Vyuo hivi vya madaktari kimsingi kuna vingine vilitakiwa visiwepo kabisa,,hawana walimu, miundombinu,nk,wanazalisha madaktari ambao kimsingi ndo wanaongoza kwa kuuwa wagonjwa,,Mfano vyuo vya udaktari vilivyo DSM vinategemea walimu wa Mhimbili kwa asilimia karibu 90, ukumbuke na hawa walimu wanamajukumu yao muhimbili,, cha kusikitisha wanafunzi wa kuanzia mwaka wa tatu wanafanya mazoezi hospitali ya mwanamwanyala, Ilala na temeke, daktari wa atakayepatikana hopo ndo wale wanaouwa wagongwa kila siku,,Kuna chuo hapo DSM kilifungiwa na TCU,,hawa wanasiasa wakatengua uamuzi wa TCU
Kuna uhaba kweli wa madaktari lakini uhaba huo usitumiwe kutuzalishia madaktari BOMU, Tujifunze kutoka RWANDA kila kukicha wanakuja ku dahii madaktari kutoka Bugando, Mbeya na Mhimbili,,
Jamani uchakachuaji kwenye mafunzo ya udakitari ni hatari mno kulinganisha na uchakachuaji katika fani nyingine! Umakini zaidi unatakiwa kwa wanaosajili vyuo.
Kwa jinsi Elimu ya Afya inavyopelekwa nchini baada ya muda kutakuwa na maafa maana walimu wanalalamika wanafunzi wabovu hawasomi. wanafunzi nao wanalalamika walimu wako busy na mambo yao ya part time na utafiti/biashara...........
ukosefu wa motisha na vifaa/dawa katika sekta ni tatizo. Ukijumlisha haya yote kupata huduma/tiba itakuwa balaa. Utatoa rushwa kwa daktari asiye na ujuzi, maana hata private clinics ni hao wanafanya kazi.