Hili ni moja yamakosa mengi ayanayofanywa na viongozi wetu, au baadhi yetu .Hatupendi kujua mzizi wa tatizo
Mwanafunzi wa chuo kikuu hajatokea tu hewani-ameanzia vidudu(chekechea/nursey school) mtaani kwao, primary kasoma Tanga, O-level kasoma Dodoma, A-level kasoma Mwanza. Chuo kikuu anakuja DSM.(mfano)
Huko kote anaruhusiwa kuvaa kwa staili yeyote kwani sio kioo cha taifa? mpaka afike chuo kikuu? Hivi nani anaona watoto wa sekondari wanavyovaa siku hizi? au kuvaa mpaka iwe siku za shule tu.
Taifa linaanzia, nyumbani, mtaani, kitongojini, kata, tarafa, wilaya, mkoa , zone, na ndio taifa!!!!! wanafunzi hawa wanatoka huko walikotoka na tabia zao, leo hii mnataka muwabadilishe CHA AJABU WENGI WANAJISAHAU WAKIDHANI HAWA NI WATOTO KUNA WENGINE WANA FAMILIA, NI BABA NA AKINA MAMA FULANI.
Kama mtoa maada alivyosema, kuna mengi ya kutatua kwa sasa, hili tumechelewa mno, maana ni dunia ya 'domokrachia' sio demokrasia, haki za binadamu-ubepari , at least tungekuwa na ujamaa wetu, enzi zile mtoto analelewa na jamii na sio baba na mama tu. Siku hizi thubutu, nyoshea kidole mtoto wa mtu uone-Morogoro mpaka wazazi wanawapiga walimu!!
Mh. Mbunge-tuanze na ngazi ya familia pengine utaona ugumu wa hili swala, anza na hapo bungeni , mawaziri wangapi na wabunge wangapi watoto wao wanaishi maisha ya 'kizungu' ?? yes -no nyingi, beach kila wikendi na baba zao huku wamevaa nguo fupi na zinatisha(eti maendeleo) , wamepata approve za wazazi wao! leo waziri unaamka usingizini! watoto wameruhusiwa na wazazi wao kuvaa nguo fupi leo hii unataka kuzuia!
pengine anzisheni uniform, au maadamu mmeanza na hili la maaskari, wekeni shift ya maaskari kila hall/residents kuzuia nguo fupi! kazi ni wale wanaotoka makwao! au au askari kushindwa uzalendo!
wakatabau