Nakuunga mkono met. Tatizo letu sisi watanzania huwa tunatarajia makubwa kwa mara moja na hii inatokana na kutoruhusu upeo wa uelewa kuwa na mawanda mapana ya fikra. Siku zote huwa tunafananisha mbuyu na mchicha bila kuhusisha umri wao, ustahimilivu na uwezo binafsi.Hata mtoto akizaliwa huwa anaanza kuendele kukua na kukomaa sehemu muhimu kwanza na baadae sehemu zingine kuendelea kuongezeka na kuimarika sasa tukitaka mtoto azaliwe na kukua na kutembea siku hiyo hiyo si tutampindisha mgongo na miguu itakuwa na matege...hebu tujaribu kuruhusu mabadiliko yachukue nafasi yake kwa utaratibu na uwezo husika wa kiuchumi, tukilazimisha sijui kama tutafika malengo halisi ya Elimu kama ambavyo wenzetu wamefikia. Halafu siku zote msomi unapotoa hoja huwa inasindikizwa na mapendekezo madhubuti ya kufanikisha utatuzi wa changamoto unayoiwasilisha na sio kutoa lawama tu...!Bravo Kaizer!Hivi Waungwana niulize tu, UDSM ilianza na wahadhiri wangapi 'wenye qualifications"na je, the other scenario, Kama isingeanzishwa UDOM, hao wanafunzi almost 18,000 wangekuwa wapi sasa hivi given the current capacaity ya public universities, na ada 'za kuruka' za vyuo vikuu binafsi?Kweli kuna mtu angetegemea, as from 2007, chuo kiwe kimeshajitosheleza kwa wahadhiri wenye qualifications, madarasa pamoja na mabweni, maktaba, vitabu vya kutosha nk?Isnt it nice to start somewhere? Ninavojua mimi, kwenye chuo kikuu kuna mchanganyiko wa wahadhiri...kuanzia tutorial assistants hadi maprofessa. Kinachoonekana sasa hivi ni kwamba maprofesa wengi wanaelekea kustaafu na hili linasababishwa na sera ya serikali (au ya WB) miaka ya 90 kufreeze ajira. Sasa wakiajiriwa wahadhiri ambao watajiendeleza wakiwa tayari kazini, at the same time kukiwa na back up ya wahadhiri kutoka nje, kuna tatizo gani?Au tunadhani kuwa vyuo vikuu "vinashuka' tu kama mana jangwani, havi-evolve over time? Unapolinganisha kwa mfano UDOM na UDSM ambayo ilianza 1964, nadhani inakuwa sio fair ....vyuo vingine duniani mfano Cambridge ni vya tangu karne!
uwezo mkubwa kupembunua mambo kama kumchangia Jk million 1 ya uchaguz? Hebu fkiria eti chuo kikuu anamalza miaka mitatu hajui nn maana ya field, wakat hata vyuo vya hotel management, tourism and tour guiding vya magomeni, kariakoo na buguruni wanafanya fieldAcheni watu wasome, hayo ndo maendeleo yenyewe. Nyie mnataka mwe na chuo kimoja kama cha enzi zile??Acheni hizo, na uhakika mtu aliyefika chuo kikuu hata kama kipo chini ya mwembe ana uelewa mkubwa wa kupambanua mambo kuliko yule wa LY.
Ni mwanzo, mara nyingi mwanzo wa kitu chochote huwa mgumu, serikali kuanzisha vyuo vikuu haija kosea. Hiyo ni hatua ya kwanza kuwa na taasisi, halafu baadaye kuwa na walimu wenye sifa. Isingekuwa hekima (kwa mawazo yangu lkn) kusubiri kuwa na walimu wenye sifa, halafu ndiyo kuanzaisha taasisi. Hapa tulipo si pabaya, hayo ulioongelea hapo juu ni marekebisho tu, na si ya msingi, walimu watapatikana tu, na ndiyo maana serikali imeanza kuajiri ma-dr na ma-prof toka sehemu yoyote ya dunia.
Ondoa shaka, Roma haikujengwa kwa siku moja, vivyo hivyo, vyuo vyetu havitaimarika kwa siku moja, ni mchakato. cha msingi ni kuwa na mipango na mikakati ambayo inazingatiwa na kufuatwa.
Unaongea saaaana bila kujua hali halisi. Hivi nani kakwambia kuwa wanafunzi wote wa udom ni wana ccm?? Fatilia mambo kwa ukaribu sio kukosoa tu. Wanataaluma wapewe heshma yao.uwezo mkubwa kupembunua mambo kama kumchangia Jk million 1 ya uchaguz? Hebu fkiria eti chuo kikuu anamalza miaka mitatu hajui nn maana ya field, wakat hata vyuo vya hotel management, tourism and tour guiding vya magomeni, kariakoo na buguruni wanafanya field
Kwa nini watanzania hawataki kuongelea mambo ya msingi kwa undani. Mfano elimu ya chuo kikuu leo inafanana na ya shule za kata. wakubwa wanatamba majukwani wameanzisha vyuo vikuu vingi kama UDOM. lakini hawaoni matatizo yaliyopo kwenye vyuo hivyo.Hakuna vifaa,Hakuna Maprofesa,majengo hayatoshi. Watu wenye Masters ndio walimu ambao nao wamesoma kwa kuunga unga tu. vyuo vikuu vya namna hii vitatufikisha wapi. Mtoto kafaulu kwa kubahatisha darasa la saba halafu kaenda shule ya kata kafaulu kwa kukairiri kaenda chuo kikuu UDOM. Hapa kweli tutasema tumezalisha msomi wa kuiomboa nchi hii katika ulimwengu huu wa utandawzi, soko la pamoja nk. Tanzania inaelekea pabaya. lakini viongozi wetu wanafurahia sifa rahisi rahisi. Wanchi nao wamelewa fikra za kipumavu za zidumu fikra za mwenyekiti. Taifa hili linahitaji mwelekeo mpya . we are in wrong boat and wrong direction.
Kaizer,
Ningependa kukujibu kuwa UDSM ilianza ikiwa na waalimu wengi tu wa kutosha kutoka Uingereza, Jamaica, na kwingineko waliokuwa well qualified. Wakati huo serikali ilijitahidi sana kuajiri the best minds there was in the academic world. Sizo hizi porojo za sasa za kujenga UDOM bila kufanya maandalizi stahiki na juzi namsikia mkulu wa CCM akijidai kuwa mwaka huu waalimu elfu 15 wanafuzu masomo. UDSM ya 60-70 ilikuwa an intellectual oasis.
Kwa nini watanzania hawataki kuongelea mambo ya msingi kwa undani. Mfano elimu ya chuo kikuu leo inafanana na ya shule za kata. wakubwa wanatamba majukwani wameanzisha vyuo vikuu vingi kama UDOM. lakini hawaoni matatizo yaliyopo kwenye vyuo hivyo.
Hakuna vifaa,Hakuna Maprofesa,majengo hayatoshi. Watu wenye Masters ndio walimu ambao nao wamesoma kwa kuunga unga tu. vyuo vikuu vya namna hii vitatufikisha wapi.
Mtoto kafaulu kwa kubahatisha darasa la saba halafu kaenda shule ya kata kafaulu kwa kukairiri kaenda chuo kikuu UDOM. Hapa kweli tutasema tumezalisha msomi wa kuiomboa nchi hii katika ulimwengu huu wa utandawzi, soko la pamoja nk. Tanzania inaelekea pabaya. lakini viongozi wetu wanafurahia sifa rahisi rahisi. Wanchi nao wamelewa fikra za kipumavu za zidumu fikra za mwenyekiti. Taifa hili linahitaji mwelekeo mpya . we are in wrong boat and wrong direction.
nakufahamu mh. We c afisa utumish wala nn,ila ntakutafuta ili 2onge vzur,maana ts too muchKweli kabisa wadau UDOM ni bomu la kufa mtu. Mimi ni Afisa Utumishi Shirika fulani hapa nchini lakini najua kabisa kuwe ukiajiri mwanafunzi kutoka UDOM utakuwa na kazi ya ziada ya kumwelekeza kupita kiasi kulinganisha na vyuo vingine sijui tatizo nini jamani wanatia huruma sana. Yaani hata kumwelekeza ajibu barua ya kiofisi tu lugha atakavyoichakachua utakaa chini usikitike. Mimi naona UDOM kuna tatizo la msingi zaidi tunavyofikiria kwani haiwezekani mtoto graduate awe kila vile kazini. Nakubali mtu huanza kazi kwa shida kwa sababu ya uzoefu lakini unategemea baada ya muda at least abadilike basi lakini kwa hawa UDOM ndugu yangu hakuna kitu. Mimi nikishaona kutoka UDOM basi naanza kujisikia huzuni walivyo vilaza.