Vyuo na mashule jiongezeni, acheni kulala

Vyuo na mashule jiongezeni, acheni kulala

bizplan

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2013
Posts
592
Reaction score
574
Jamani hebu kuweni pro active basi hata kidogo. So far shule na vyuo haijulikani lini vinafunguliwa, kwanini msijiongeze kutumia mifumo ya mawasiliano kufundisha kipindi hichi?

Nafahamu baadhi ya shule za msingi English medium wameanza kufundisha watoto kwa kutumia Zoom; you cant imagine unamsetia mtoto laptop masomo yanaendelea. Japo watoto wanashindwa ku-intereact vizuri na system lakini kwa kweli wanasoma.

Tukija vyuoni, unashangaa vyuo vingi nchini wamefunga and nothing goes on. Jamani jiongezeni.

Nilisikia wanafunzi wa chuo cha uhasibu Arusha kuwa wanaendelea na masomo kwa njia ya mtandao na kwamba masomo yakiruhusiwa ni kuja kufanya mitihani etc.

Vyuo msikae na kupoteza muda, kwa kuwa wanafunzi wa vyuo ni rahisi kuinteract na systems kama zoom etc tumieni huu muda wanafunzi wasome.

Yawezekana zikawepo changamoto za vifurushi vya internet na mengineyo, lakini ni muhimu vyuo vifanye juu chini kutatua changamoto hizo. Cha muhimu wanafunzi wasome katika kipindi hiki badala ya kupoteza muda.
 
Sijui kama itakua affordable kwa kila mwanafunzi. Wanafunzi wengine wapo huko kwao wanavuna mpunga.
 
Wakirudi wanakuja kufanya mitihani kutoka kwa nani? Labda test za hapo chuoni kwao. Mwenye mamlaka na mitihani ndo aloamua kufunga na ratiba nyingne zitazofuata atapanga yeye.

Ko watu wasome engineering mtandaoni kweli? Basi wazame tu youtube

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa vyuo vipo ama chini ya TCU ama NACTE.

Hawa watu walitakiwa kutoa mwongozo ama ramani kuonyesha iwapo ratiba zao za mihula na mitihani zinaweza kubadilika.

Ila ni mabaraza yaliyojaa watu waliojichokea na wanasubiri kufungia vyuo tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nahisi Kuna bahadhi ya fani ni ngumu kuendesha mafunzo mtandaoni huku kukiwa na ubora wa elimu, hasa za kazi za vitendo.

CCM DAMUDAMU!!!,CHAMA CHA MAMA &BABA

Ni kweli baadhi ya fani ni ngumu. Ila wao ni wasomi lazima waje na suluhu ya changamoto hii ili wasome hata katika wakati huu mgumu.
 
Kwa vyuo vipo ama chini ya TCU ama NACTE .

Hawa watu walitakiwa kutoa mwongozo ama ramani kuonyesha iwapo ratiba zao za mihula na mitihani zinaweza kubadilika.

Ila ni mabaraza yaliyojaa watu waliojichokea na wanasubiri kufungia vyuo tu

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwa kweli wakae wafanye jambo kwenye hili.

Mfano vyuo vya South Africa, wengi sasa hivi wanafanya juhudi kuhamia online ili kuendelea na masomo.
Bila shaka miongozo walishapeana.
 
bizplan,
Hiyo kitu ni mzuri ila je wajua taifa lako lilivyo? Kuna vijiji mpaka leo hii network ni shida au akuna kabisa au wapo mbali na dunia hii kabisa.
 
Ni wazo zuri lakini kuna factors nyingi za kuzingatia. Sio kila kaya inamiliki laptop ya kuweza kuidedicate kwa mtoto tu. Kuna kaya zenye wanafunzi zaidi ya mmoja ambapo pia ni changamoto kuweza ku allocate resources za kusomea online kwa kila mtoto.

Wengi ya wazazi ni wafanyakazi, kurudi kwao ni jioni. Ni swala moja kukagua homework lakini kusimamia masomo yote hiyo ni changamoto.

Mwisho wa yote hiyo system ni rafiki kwa wale wa English Medium maarufu kama academy, kina Kayumba nao unadhani wana miundombinu ya kuwezesha hilo?

Hili janga limekuja kuvumbua mengi ikiwemo udhaifu na uduni wa mfumo wetu wa elimu.
 
Inawezekana wakajaribu kufanya hivyo.. lakini chamgamoto ni kubwa sana kama upatikana ji wa network nchi nzima, wanafunzi wanatokea sehemu zote za Tz na kuna sehemu kupata hata 3G ni kazi sana .. kuna wanafunzi hawana hio laptop unayoiongelea, au hawana hata smartphone.

Kuna watu hawana hela ya bundle n.k n.k.
Changamoto ni nyingi sana..

Mimi naona serikali itoe takwimu za ugonjwa tuone tumefika wapi; kama hali ni nzuri basi tunaweza kufungua vyuo kwanza kwa awamu.. yaani tukatumia system kama ya Mzumbe university watu wanasoma kwa kupokezana. Nusu wanaenda chuo nusu wanabaki ili kupunguza misongamano.
 
Ni kweli baadhi ya fani ni ngumu. Ila wao ni wasomi lazima waje na suluhu ya changamoto hii ili wasome hata katika wakati huu mgumu.
Hivi ni famlia ngapi zenye uwezo wa kupata laptop kwa ajili ya mtoto/watoto kujisomea kwa njia ya mtandao? Bado tuko nyuma sana katika eneo hili. Pia kuna chngamoto ya mtandao ili kupata masomo kwa njia ya mtandao.
 
Ni kweli baadhi ya fani ni ngumu. Ila wao ni wasomi lazima waje na suluhu ya changamoto hii ili wasome hata katika wakati huu mgumu.
Fani zote za sayansi haziwezi kufanywa kwa izo njia za kutoa notes na video alafu udhani utapata watu apo .unadhani utapata madoctors, engineers,watu wa geometric , surveys na wengine wengi wa sayansi bila ya mafunzo ya vitendo na kuwafanyia assessment kama lecture.labda izi za ngonjera na haya Mambo ya uhasibu pengine

CCM DAMUDAMU!!!,CHAMA CHA MAMA &BABA
 
Ni wazo zuri lakini kuna factors nyingi za kuzingatia. Sio kila kaya inamiliki laptop ya kuweza kuidedicate kwa mtoto tu. Kuna kaya zenye wanafunzi zaidi ya mmoja ambapo pia ni changamoto kuweza ku allocate resources za kusomea online kwa kila mtoto.

Wengi ya wazazi ni wafanyakazi, kurudi kwao ni jioni. Ni swala moja kukagua homework lakini kusimamia masomo yote hiyo ni changamoto.

Mwisho wa yote hiyo system ni rafiki kwa wale wa English Medium maarufu kama academy, kina Kayumba nao unadhani wana miundombinu ya kuwezesha hilo?

Hili janga limekuja kuvumbua mengi ikiwemo udhaifu na uduni wa mfumo wetu wa elimu.
SAFI SANA
 
Back
Top Bottom