Pale inatakiwa overhauling kali, nimesoma pale miaka minne lakini hali ni kutisha kadri siku zinavyosonga mbele. Inatia aibu sana kama hakuna la maana sehemu yeyote!!
Maji bado tunabahatisha kuyapata,
umeme bado tunabahatisha,
elimu bado kabisa pamoja na kufahamu umuhimu wake,
barabara/miundo mbinu kwa ujumla bado,
utendaji wa kila sehemu ndo hivyo tena.
Pamoja na kufahamu yote hayo kuwa yana umuhimu bado viongozi wetu hawataki kuona umuhimu wa makusudi/kujitoa mhanga ili kuokoa jahazi kwamanufaa ya taifa mbeleni.