Vyombo vyetu vya habari ni hatari kwa amani yetu!

Mnyampaa

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
244
58
Ndugu wana JF, Ni falsafa yangu inanituma kuamini kuwa ipo siku hali ya UTULIVU katika nchi hii itakwisha kutokana na dalili ninazoziona na mwisho AMANI tuliyonayo kutoweka. Kwa mtazamo wangu hali hii yaweza kutokea kutokana na mchango mkubwa wa vyombo vya habari katika kushabikia FUJO na MATUKIO yanayohatarisha upotevu wa amani katika jamii yetu aidha kwa maslahi ya kikundi fulani cha watu au maslahi binafsi ya chombo husika cha habari.

Hisia zangu hizi nazipata kutokana na vyombo vya habari vinavyoendelea kuripoti kwa ushabiki tukio la wabunge wa CHADEMA kumkamata Mkuu wa Wilaya ya Igunga kutokana na kilichosemwa kufanya kikao katika eneo lililokaribu na mkutano wao wa kampeni.

Nisingependa kujadili jinsi suala hili lilivyogeuka kuwa la kidini, kisiasa, kiutamaduni wala kimaadili bali nataka kuzungumzia jinsi vyombo vya habari hususan redio na magazeti vinavyoendeleza mjadala kuhusu suala hili. Ingawa mimi si mwandishi wa magazeti na wala si mtangazaji wa redio ila ni msomaji na msikilizaji nahisi kuathirika na mijadala inayoendelea na nadhani kama mijadala hiyo haina mipaka basi vyombo hivi vitaleta dhahama kwa taifa letu kwani ladha tunayoipata kutoka kwenye hiyo mijadala ni ya kujenga chuki na mfarakano wa watu ndani ya jamii.

Naomba nitumie mfano mmoja tu wa mjadala wa watangazaji wa CLOUDS FM katika kipindi cha JAHAZI kuonesha namna watangazaji wetu wasivyo na uelewa wa kutosha juu ya athari za kile wanachokizungumza kwa jamii ya watu wanaowasikiliza na mustakbali wa taifa letu. Katika Kipindi cha Jahazi cha tarehe 21/9/2011 kwenye redio hiyo ulizuka mjadala wa kauli mbalimbali zilizotolewa na taasisi za kiislamu na wanawake juu ya Mkuu wa Wilaya ya Igunga kuvuliwa hijabu katika tukio nililoelezea hapo juu.

Katika mjadala huo watangazaji wa kipindi kama watanzania wengine walilaani sana kitendo hicho. Kwangu mimi tatizo lilikuwa hapa; baada ya mjadala kuendelea nilimsikia mtangazaji mmoja anayefahamika kwa jina la KIBONDE akisema, "HIVI WAISLAMU NAO WAKIAMUA KWENDA KANISANI, WAKAMSUBIRIA SISTA AKITOKA NA KUMVUA KILEMBA CHAKE HAPO UNATEGEMEA NINI? Mwenzake alimuambia aah huko sasa unakwenda mbali zaidi hebu tupate kwanza tangazo halafu tutaendelea. Kibonde akalazimisha kuendeleza mjadala huo kwa sababu alitaka kujustify kile alichosema. Kutokana na mfano huu halisi katika redio moja tu na vichwa vya baadhi ya magazeti mbalimbali imenipa ufahamu zaidi juu ya mchango wa wanahabari kwa kile kilichotokea Rwanda mwaka 1994 na kwingineko.

Naomba kumaliza kwa kutoa angalizo

Kitendo alichofanyiwa Mkuu wa Wilaya si jambo la heshima, ustaarabu na haki katika macho ya wastaarabu hata kidogo kwani kuna sheria na taratibu za kistaarabu kwa kutumia vyombo vinavyohusika ukizingatia tuhuma zinazotolewa.

Siamini hata kidogo kuwa watuhumiwa walienda  kumkamata na kumvua hijab Mkuu huyo wa Wilaya kwa kuwa yeye ni Muislamu na wao ni wakristu kama ambavyo Kibonde alivyotaka watu waamini kwa kulinganisha tukio hilo na Sista wa Kikristo.

Kuna haki zote kwa taasisi au chombo chochote kulaani jambo ambalo kwa imani au maadili linaonekana kuwa si jema katika jamii kama makundi mbalimbali yalivyofanya na nina imani hatua hiyo haina nguvu ya kisiasa.

Kwa waandishi na watangazaji ambao hufanya kazi zao kwa hisia zaidi bila kujali maadili ya kazi zao na hususan kupima athari za yale wanayoyaandika au kutangaza kwa audience yao ni hatari sana kwani hupelekea mwanzo wa chuki na uvunjifu wa amani kutokana na hisia wanazopandikiza kwa watu. Kauli ya Kibonde inaleta chuki baina ya dini zetu mbili kwa kuaminisha watu kuwa jambo hili linahusisha dini zetu na hakuwa na sababu yoyote ya kuingiza ukristu katika mada husika lakini kwa kutojua kwake alifanya alichofanya.

Namalizia kwa kusema, "Ana busara mjinga aliye kimya kuliko mwerevu anayebwabwaja"

MUNGU IBARIKI TZ

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom