Vyombo vya habari vya watuhumiwa wa mihadarati na watetezi wao visifanye kazi hadi kesi ziishe

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
Vyombo hivi kuendelea kufanyakazi huku watuhumiwa wakiwa bado hawajamalizana na kesi zao ni kosa kwa sababu vitaweza kuathiri mienendo ya kesi hizi.
Naongelea:
1. Free Media ya Freeman Mbowe
2. Habari Coorporation ya Manji
3. Magazeti yote yanayomilikiwa na Jenerali Ulimwengu anayemtetea Freeman Mbowe Mahakamani
4. Redio EFM
Na vingine kama hivyo.
 
Mkuu vipi tena? Mbona kama vile una chuki imetanda mpaka unashindwa kufikiria na kuamua?
Unaona sasa ulichokuja kuandika?

Au kwakua hivyo vyombo vinaulizia uhalali wa jina Bashite na matokeo yake?
Kumbe na wewe unajua ndivyo vinahoji uhalali wa elimu ya Makonda? Ehee kwanini leo ambapo Makonda amebainisha kuwa Mabosi wa Vyombo hivi ni wauzaji na watumiaji wa Mihadarati?
 
Vyombo hivi kuendelea kufanyakazi huku watuhumiwa wakiwa bado hawajamalizana na kesi zao ni kosa kwa sababu vitaweza kuathiri mienendo ya kesi hizi.
Naongelea:
1. Free Media ya Freeman Mbowe
2. Habari Coorporation ya Manji
3. Magazeti yote yanayomilikiwa na Jenerali Ulimwengu anayemtetea Freeman Mbowe Mahakamani
4. Redio EFM
Na vingine kama hivyo.

Uzuri hata RC naye ni mtuhumiwa wa Madawa ya kulevya na usafishaji noti,maana wale drug lords wenyewe ndiyo Marafiki zake wakubwa na wala hajwagusa kuwataja.

Pili kwanini alitumia njia mbaya kabisa ya kuwakimbiza hao drug lords au kuwafanya waondoe shehena yao kwa kusingizia watu wengine??

Ikiwa hiyo unayosema ni Rahisi basi hata magazeti ya mtuhumu yasifanye kazi na RC pia asimamishwe kazi kupisha uchunguzi
 
Kumbe na wewe unajua ndivyo vinahoji uhalali wa elimu ya Makonda? Ehee kwanini leo ambapo Makonda amebainisha kuwa Mabosi wa Vyombo hivi ni wauzaji na watumiaji wa Mihadarati?

Elimu ya Makonda ilianza kuhojiwa toka enzi hata kabla hajawa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni.

Naona mko busy kumsafisha naye ni wale wale walezi wa wauza Unga Masogange,GSM na Kinje
 
Wewe unachofanya hapa ni umbea. Kawataje hao kama RC alivyofanya au peleka kwa Kamishna Siang'a
 
Hii mada ni ya Media za Watuhumiwa na Mihadarati, hii ya Makonda si mmeshatoa mapovu sana japo mmeambulia patupu? Nenda kwenye mada ya Makonda ina karibia page ya 70 wambea wenzako wako huko
 
Wewe unachofanya hapa ni umbea. Kawataje hao kama RC alivyofanya au peleka kwa Kamishna Siang'a

Awataje nani wakati weshatajwa na Mapunda wao??Huyo Masogange si alishikwa SA na mzigo wa Kinje?Mnadhani hatuna akili??
 
Hata chama cha chadema hiki ndio Kimbilio la wauza Madawa kwa sasa
Hahahahah usiongozwe na jaziba kupita kiasi maana habari ni haki ya kila mtanzania wewe unaposema kuendelea kuminya uhuru wa habari nashindwa kukuelewa maana hata hapa jamii forum penyewe kuna kesi ipo mahakamani kama watafanya kama hivyo uonavyo utatolea wapi hayo maoni yako ya kutaka kudidimiza uhuru wa kupashana habari?
 
Awataje nani wakati weshatajwa na Mapunda wao??Huyo Masogange si alishikwa SA na mzigo wa Kinje?Mnadhani hatuna akili??
Unamtaja masongange ambaye tayari ameshakamatwa? Kama angekuwa rafiki wa RC angekamatwa? Mtatapatapa sana nyie lakini Mungu kamshusha Makonda kuwaweka hadharani wabwia unga mapapa ambao walishindikana. Leo wanahangaika Mahakamani wakifikri watapona. Mahakama zikiwaachia tutawazomea huku mitaani mpaka watakoma.
 
Kumbe na wewe unajua ndivyo vinahoji uhalali wa elimu ya Makonda? Ehee kwanini leo ambapo Makonda amebainisha kuwa Mabosi wa Vyombo hivi ni wauzaji na watumiaji wa Mihadarati?
Hata hivyo unajua kama Ijumaa limeanza kufuatilia hilo swala?
Na Ijumaa ni Global Publi.
 
Hahahahah usiongozwe na jaziba kupita kiasi maana habari ni haki ya kila mtanzania wewe unaposema kuendelea kuminya uhuru wa habari nashindwa kukuelewa maana hata hapa jamii forum penyewe kuna kesi ipo mahakamani kama watafanya kama hivyo uonavyo utatolea wapi hayo maoni yako ya kutaka kudidimiza uhuru wa kupashana habari?
Mbowe +Wema= Bangi2
 
Na wakishinda kesi mtawalipa gharama zote kwa hasara watakayoipata baada ya iufunga matangazo kwa muda husika...???

Hivi sisiemu akili zenu wakati mwingine mnaziweka wapi?? Au huwa mnafikiri kwa kutumia kiungo gani cha mwili tofauti na ubongo??
 
Hakuna mtuhumiwa wa Mihadarati atalipwa hata shilingi ashinde asishinde. Hii ni awamu ya tano.
 
Unamtaja masongange ambaye tayari ameshakamatwa? Kama angekuwa rafiki wa RC angekamatwa? Mtatapatapa sana nyie lakini Mungu kamshusha Makonda kuwaweka hadharani wabwia unga mapapa ambao walishindikana. Leo wanahangaika Mahakamani wakifikri watapona. Mahakama zikiwaachia tutawazomea huku mitaani mpaka watakoma.

Amekamatwa baada ya akina Wema kulalamika uliambiwe yule nyumba ndoga yake alimtaja??Sema ukweli Paul Makonda aka Bashite alimtaja??Kwani MAkonda alikuwa hajui tuhuma za Masogange??Je hajui tuhuma za GSM kuwa ni watakatishaji wa pesa na wengine wao ni drug lords??Anajua lakini bado anakubali kufadhiliwa na kundi hilo,ni aibu kwake na kwa aliyemteua.
 
Back
Top Bottom