GHIBUU
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 4,432
- 3,011
Wakati mwingine wananchi wanashindwa kufahamu weledi wa vyombo vya habari vya Tanzania, ukweli ni kwamba haviwasaidii katika kupambana na dhuluma, uonevu dhidi ya matumizi ya mabavu ya watawala.
Na hapa wanapata picha kuwa vyombo vya habari vya Tanzania, vyenyewe vinajiondoshea sifa ya kuwa muhimili wa nne wa nchi kwa sababu vinafanyakazi kwa hofu, huku wanajua kwamba kinachofanyika si haki, hakikubaliki, bali vinasidia mabavu ya watawala katika kuwadhulumu wananchi.
Vyombo vya habari vya Tanzania, wakati mwingine vinatia kichefu-chefu ni aibu au niseme ni vichekesho vitupu, vinafanyakazi za hovyo-hovyo, haviwasaidii wananchi kutetea haki zao zinapoporwa na watawala wasiyotaka kuondoka madarakani.
Vyombo vya habari vya Tanzania, vinashiriki katika kuhalalisha dhuluma na kusema uoga. Vinahalalisha haramu iliyolaaniwa na ulimwengu mzima. Hii inamaanisha hisia za umasikini, usaka tonge, tamaa na woga kwa watendaji wa vyombo vya habari.
Yaliyofanyika Zanzibar juzi katika kile kilichoitwa ‘UCHAGUZI WA MARUDIO’ ni mambo yaliyostahili kupingwa na baadhi ya vyombo vya habari vilivyokuwa havina mnasaba/uhusiano na dola/CCM.
Uchaguzi wa Marudio, ulikuwa haustahili kufanyika kama vyombo vya habari vinginejitolea muhanga kuupinga ili kusaidia wananchi wa Zanzibar, kutetea haki yao ya kidemokrasia, kama yalivyofanya mataifa ya nje kupitia waangalizi wake wa uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka jana.
Wallahi, hakuna hata mtu mmoja asiyehoji/asiyelalamika kuwa, Dk Shein ametumia mfumo kamili wa udikteta kuendelea kutawala, huku vyombo vya habari vikimpamba na vingine kujaza hadithi nyingi za uogo. Kuacha kueleza ukweli juu ya uchaguzi wote.
Televisheni, mbali ya zile za serikali ya CCM, zimeonyesha live tukio la kuapishwa kwa Dk Shein, huku wanajua kwamba uchaguzi wa marudio ni batili wa kipuuzi, haukuwa na sifa ya uchaguzi (ni uchaguzi wa ccm) tu.
Tangu mwanzo, utaratibu mzima wa uchaguzi haukuwa wazi na wa kueleweka kwa wahusika na haukuhakikiwa na chombo chochote. Ulijaa hila/mbinu/ujanja na kama mchezo wa hadithi za Bunuasi. Propaganda na kuminywa kwa haki kusikoelezeka, bila kukosolewa na hata vyama vilivyoshiriki huo uchaguzi wa marudio.
Badala yake vyombo vya habari vilitakiwa kulaani vikali kitendo kilichofanyika Zanzibar na siyo kusifia upuzi hadharani. Kwa hili vyombo vya habari vimepotoka sana. Kwa kifupi Tanzania, vyombo vya habari bado kabisa ni kivuli. Benjamin Mkapa wakati akiwa rais, aliwahi kuvipuuza.
Maalim Seif, aliwahi kusema kuwa Dk Shein tayari katika uchaguzi wa marudio ana matokeo yake mfukoni kutokana na ushauri wa Jakaya Kikwete na kuungwa mkono na Magufuli kwa kumimina vikosi vya Jeshi Zanzibar.
Naamini mia fil mia kuwa wananchi wa Zanzibar na wapenda haki popote walipo DUNIANI wanalaani kitendo kilichofanywa na vyombo vya habari vya Tanzania kutokana na kushadidia ukandamizaji wa haki kuviza mamuzi yao ya demokrasia ya Oktoba 25, 2015.
Wazanzibari wanapaswa kufanya maamuzi magumu kwa kugomea kupuuzilia mbali kuto-kununua magazeti yote yanayochapishwa Tanganyika, likiwemo Mwananchi, Nipashe na kadhalika kwa sababu yameshindwa kutumia uhuru wa habari kuwasaidia katika kupambana na utawala dhalimu wa Dikteta, Ali Mohamed Shein.
Kwa upande wa BBC-Swahili na Sauti ya Ujeruman ‘Deutsche Welle (DW) Swahili, ni muda mrefu nimeacha kusikiliza radio hizi yaani naweza kusema sikumbuki ni miaka mingapi sasa sisikilizi. Juzi iliyotokezea tu nikasema hebu nisikilize.
BBC-Swahili wanafaa kupongeza maana habari kuhusu Dk Shein kuapishwa hawakuitangaza kabisa. Ujerumani, DW-Swahili waliitangaza kwa mapana na marefu, kitu gani kiliwavutia au walikiangalia, sijui.
CUF, tayari wamesema kwamba hawamtabui Ali Mohamed Shein na serrikali yake, kila Mzanzibari, anayeumizwa na nchi yake achukie utawala wa Kidekteta wa Ali Mohamed Shein.