Vyombo vya habari na ushabiki wa hatari

Vyombo vya habari na ushabiki wa hatari

EJM_

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2011
Posts
3,836
Reaction score
2,108
Siku za hivi karibuni kumekuwa na kile wanachokiita uhuru wa vyombo vya habari hapa nchini. Hali hii imepelekea kuanza kukosekana kwa maana halisi ya vyombo vya habari na jukumu lake kubwa kwa Taifa. Moja ya Radio ambazo mi huwa nasikiliza sana ni Clouds FM (Kwakuwa ndio radio pekee inayosikika vyema huku kwetu) lakini katika siku za hivi karibuni naanza kuhisi kama imeanza kukosa muelekeo hasa linapokuja suala la kutofungamana na upande wowote.

Mfano mmoja mzuri ni matukio mawili makubwa yaliyotokea siku za hivi karibuni;

  1. Mgogoro wa gesi ya Mtwara; Mi nilifikiri kazi kubwa ya chombo cha habari ingekuwa kuziweka pamoja fikra za pande zote na kuwaleta wataalam mbalimbali wenye mawazo tofauti ili kujenga picha ya balanced news kuliko kufanya kampeni ya kipuuzi kama waliyokuwa wanaifanya Clouds FM. Sikuwahi kusikia hata siku moja hao Clouds wakiwauliza watu wa Mtwara ni hasa walikuwa wanakitaka, mwisho wakaanza kutangaza Mtwara hawataki gesi ije Dar es salaam, je ni kweli hawataki gesi ije Dar es salaam?
  2. Suala la Katiba; Mimi naamini kwamba ni kweli kila raia wa Tanzania ana uhuru wa kutoa maoni yake hasa kwenye suala muhimu kama la katiba, lakini ni lazima uangalie ni wapi unatoa hayo maoni yako, kwa namna gani unayatoa na kwa watu gani. Unapotoa maoni kwenye radio tena kwa kuwakashifu wanaotoa maoni tofauti na yako kama anavyofanya kaka yangu Kibonde mara nyingi sio tu kwamba nina wasiwasi kama maadili yanaruhusu bali pia yanatengeneza chuki zisizokuwa na msingi kwa wasikilizaji.

Katika hili nahisi kuna umuhimu wa kuangaliwa vizuri kwa matumizi ya vyombo hivi vya habari, tumeshuhudia mara kadhaa sasa zikianza kutumwa messeji za kuwatukana hawa watangazaji. Hii ni picha ya namna gani chuki na uhasama unajengeka kutokana na yale wanayoyasema kupitia radio au vyombo vyao mbalimbali vya habari. Tukumbuke mauaji ya Rwanda, vyombo vya habari vilichangia kwa kiasi kikubwa sana, tusipoangalia na sisi tunaelekea huko.

Kama vyombo vya habari vifanye kazi zao na sio kuwa mashabiki kwani hii ni hatari kwa amani na maendeleo ya Taifa letu. Nikiona habari fulani kwenye Uhuru na Mzalendo au Tanzania Daima, TBC na zile zenye muelekeo huo sishangai sana kwasababu watu wote wanajua hivi ni vyombo vya propaganda lakini sio wale wanaojiita hawafungamani na upande wowote huku wakifanya tofauti.

Ni mtazamo wangu tu.............
 
Nakushauri kuanzia sasa anza kuangalia cnn,aljazeera,sky news,bbc na nyinginezo kwani hizi za kibongo nyingi zinaegemea upande fulani kukidhi matakwa ya wakubwa wao.

Ile dana ya kuwa vyombo vya habari ni mhimili wa nne wa dola inaanza kukosa maana, na inasababishwa na hawa jamaa wanaokuwa wanafnya kazi bila kuzingatia maadili ya kazi....
Nafikiri kuna haja ya kudefine upya mipaka ya uhuru wa vyombo vya habari
 
Radio ya WAFU,,, yumo kuwadi wao humu anaitwa Nyani Ngabu ataibuka tu kutetea
 
Sio clouds tu na magazeti kama majira na mtanzania yamekuwa magazeti pendwa na kwamza majira cjui kama wanauza.
 
Si uache kusikiliza, hii ni ya kiudaku zaidi.

Mkuu unaweza kabisa kuacha kuisikiliza lakini madhara yatokanayo na hiyo sumu hutayakwepa; nadhani ndilo hasa angalizo la mleta mada. Kwa mfano, unaweza kuacha kusikiliza Radio Imaan au kusoma magazeti kama Al-Nuur lakini wakati wewe "ukisusa" kuna maelfu wanasikiliza na kusoma. Unaweza kabisa ukampuuza Sheikh Ponda na choko choko zake wala usikaribie mihadhara yake lakini kilichotokea Mbagala na kwingineko kinajieleza wazi.

Hivyo, suluhisho sio kususa bali kutafuta namna ya kudhibiti taarifa potofu na propaganda chafu kwa umma iwe kupitia vyombo vya habari au njia nyingine yoyote ingawa pia kwa upande mwingine nakubali kwamba nani na vipi taarifa itafsiriwe kama potofu au propaganda chafu nalo ni tatizo lingine.
 
Sio clouds tu na magazeti kama majira na mtanzania yamekuwa magazeti pendwa na kwamza majira cjui kama wanauza.
Hahahahaaa magazeti pendwa
 
Nakushauri kuanzia sasa anza kuangalia cnn,aljazeera,sky news,bbc na nyinginezo kwani hizi za kibongo nyingi zinaegemea upande fulani kukidhi matakwa ya wakubwa wao.

Hawa ndo awafai kabisa kila siku wanatoa habari mbaya mbaya juu ya Afrika. Idhaa zao zote kule Ulaya zinatoa taarifa za kuonyesha kuwa Afrika ni mahala pa matatizo ya kila namna hakuna jambo jema linalofanyika Afrika.

Ziangalie lakini chuja nyingi ya habari zao.
 
Nakushauri kuanzia sasa anza kuangalia cnn,aljazeera,sky news,bbc na nyinginezo kwani hizi za kibongo nyingi zinaegemea upande fulani kukidhi matakwa ya wakubwa wao.

Si kweli, hizo ni blah blah ambazo hazina msingi wowote, kwani mmiliki wa chombo cha habari toka lini akashiriki moja kwa moja kuhakiki content ya habari/ kipindi kabla hakijakwenda hewani? tuache ushabiki usio na msingi jaman, alaah!
 
Sijaona mantiki ya mwanzisha thread kuja kulalamika hapa. Peleka malalamiko yako sehemu husika ili hiyo Clouds FM na huyo Kibonde washughulikiwe vinginevyo itakuwa inaSound kama chuki binafsi.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Mkuu, huo ulikuwa ni moja ya mifano tu na kimsingi haikuwa inalenga kuonyesha chuki kwa mtu lakini nimetoa mfano ambao naamini wengi watakuwa wameusikia tofauti na ningesema "Nilimsikia Adam Mchomvu ambaye alikuwa anaplay mwenyewe maoni ya watu wanasema kitu kingine kuhusu sakata ya gesi Mtwara halafu yeye kwenye ku sum up anasema wengi wamesema tofauti na maoni aliyoplay" Sikusema hii coz naamini muda wa kipindi chake wengi tuko makazini na hatusikilizi radio.

This is not personal ni kitu cha kuangalia maslahi ya Taifa mkuu
 
Ile dana ya kuwa vyombo vya habari ni mhimili wa nne wa dola inaanza kukosa maana, na inasababishwa na hawa jamaa wanaokuwa wanafnya kazi bila kuzingatia maadili ya kazi....
Nafikiri kuna haja ya kudefine upya mipaka ya uhuru wa vyombo vya habari

.
Na hapa ndipo panaponipa wasi wasi mkubwa juu ya vijana kukabithiwa vyombo vya maamuzi. Hawatakawia kusababisha vita ya wenyewe kwa wenyewe. Wabaki kwanza kwenye kazi za misuli mpaka fikra zao zikomae na kuona mbali zaidi ya mchumba tu. Huyu kibonde wa clouds ni hatari mara kumi ya radio imani.

Wale ambao wana access na vyombo vingi zaidi vya habari wanaweza kutupa mifano mingi zaidi (Huu wa Kibonde na Clouds ni mmoja wapo tu ya mingi)
 
.
Na hapa ndipo panaponipa wasi wasi mkubwa juu ya vijana kukabithiwa vyombo vya maamuzi. Hawatakawia kusababisha vita ya wenyewe kwa wenyewe. Wabaki kwanza kwenye kazi za misuli mpaka fikra zao zikomae na kuona mbali zaidi ya mchumba tu. Huyu kibonde wa clouds ni hatari mara kumi ya radio imani.
.
umenena kweli mkuu.........
 
Mkuu, huo ulikuwa ni moja ya mifano tu na kimsingi haikuwa inalenga kuonyesha chuki kwa mtu lakini nimetoa mfano ambao naamini wengi watakuwa wameusikia tofauti na ningesema "Nilimsikia Adam Mchomvu ambaye alikuwa anaplay mwenyewe maoni ya watu wanasema kitu kingine kuhusu sakata ya gesi Mtwara halafu yeye kwenye ku sum up anasema wengi wamesema tofauti na maoni aliyoplay" Sikusema hii coz naamini muda wa kipindi chake wengi tuko makazini na hatusikilizi radio.

This is not personal ni kitu cha kuangalia maslahi ya Taifa mkuu

Kwa upeo wako wa akili, unafikiri kuanzisha kwako huu uzi hapa kutabadilisha kitu gani? Ninachosema mimi kama ni kweli unaona kuna baadhi ya vyombo vya habari vinakiuka maadili, nenda na ushahidi kwenye vyombo husika ili washughulikiwe.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Labda kuna tatizo kwenye sylabus ya uandishi wa habari kwa maana kwamba hakuna kitu kinaitwa professionalism.Na pia inawezekana waandishi au watangazaji wengi hawajapitia shule za uandishi wa habari.Haya ni maoni na fikra zangu tu.
 
Kwa upeo wako wa akili, unafikiri kuanzisha kwako huu uzi hapa kutabadilisha kitu gani? Ninachosema mimi kama ni kweli unaona kuna baadhi ya vyombo vya habari vinakiuka maadili, nenda na ushahidi kwenye vyombo husika ili washughulikiwe.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
Mkuu nafikiri kuna kitu hujakielewa au unalazimisha kutokukielewa. Dunia ya miaka ya enzi hizo sio Dunia ya sasa, Dunia ya sasa imejawa na utandawazi unaopelekea kuwa rahisi kufikisha ujumbe sehemu husika. Kwa mfano, leo kuna mchakato wa katiba mpya hapa nchini, unaweza kwenda kutoa maoni yako kwa kina judge warioba uso kwa uso lakini pia unaweza kutoa maoni kupitia Facebook na yakawafikia. Cha pili ni kwamba kuundwa kwa majukwaa ya kijamii kama hayo ni kutanua wigo wa majadiliano ya mambo mbalimbali na kupitia majukwaa hayo ambayo yanahusisha wahusika mbalimbali mabadiliko yanaweza kufanyika bila kufuata "Very conservative way" unayoifikiria wewe.

Jukwaa hili ni moja ya sehemu ambazo zinaheshimiwa sana na kwa siku za hivi karibuni limekuwa moja ya vyanzo vikubwa vya habari na taarifa hapa nchini. Majadiliano mengi yanayotokea hapa hufika kwa walengwa kwa haraka zaidi kuliko kuandika barua ya kwenda MCT na kwingineko unakofikiria. Soma alama za nyakati mkuu....
 
Vimeanza kuwa vyombo vya hatari,badala ya kuwa vyombo vya habari.
 
Mkuu,

It seems like umekariri maisha na wewe ndiye ambaye unashindwa kusoma alama za nyakati kwasababu kama ungekuwa unasoma alama za nyakati ungeelewa kwamba Kibonde na Clouds FM hawajaanza kulalamikiwa leo wala jana lakini hakuna mabadiliko yeyote sanasana wanazidisha. Kama ulimsikiliza jana kwenye kipindi cha Jahazi utaelewa ninachomaanisha ninapokwambia wanazidisha.

Soma alama za nyakati, hii njia ya kulalamika kwenye haya majukwaa imeshaFail.

Back
Top Bottom