Vyombo vya habari na tuhuma ya uongo

VIKWAZO

JF-Expert Member
Apr 9, 2011
1,899
580
Salamu wanaJF,
Nianze kwa kusema nasikitishwa sana na TABIA ya VYOMBO vya habari nchini kutuhumia kwamba ni waongo tena WAZIWAZI hasa na hawa VIONGOZI wa KISIASA (kwa wiki hii tu Spika na Mbunge wa Nzega wamevihita vyombo mbalimbali vya habari waongo) lakini cha ajabu hakuna hatua zinazochukuliwa na vyombo vinavyotuhumiwa kwamba ni WAONGO,

Leo nilipokuwa napitia bandiko moja humu JF kuhusu mgogoro wa kidini nchi, viongozi wa kidini walisema kwamba ili TATIZO limekuwa kubwa kwa sababu SERIKALI imekuwa IKIPUUZA matukio yanayoleta uchochezi wa kidini,
Nakubaliana kabisa na madai wa hao viongozi kwamba kila kitu kinahita TIMING, na matatizo yakihachwa na kuendelea matokeo yake ni kwamba wakati wa kujaribu kurudisha hali sana huko mbeleni inakuwa ngumu zaidi maana tatizo limeota mzizi,
kwa watu waliopitapita kwenye umande wanajua THAMANI YA MUDA [TIMING],

MADHARA YA HIZI KAULI
1.) Kwa sababu vyombo vya habari zinatuhumiwa uongo na vinakaa kimya basi watu wataanza kuchukulia kwamba wahandishi wote ni waongo, hivyo ni vyema kupuuza habari zao
2.) Taaluma ya uhandishi itadharaulika
3.) Democrasia nchini itadumaa maana bila kuwa na story media house upatikanaji wa habari utadumaa na kukosekana kwa taarifa ni chanzo kikubwa cha democrasia kudumaa maana watu watafanya maamuzi (hasa upigaji kura) bila kuwa na taarifa sahihi.
4.) Maadui wa wanahabari watanufaika kwa kuendeleza huu mziki kwamba vyombo vya habari waongo.

MWISHO
WanaHabari jitambueni, msikubali kuitwa majina ya ovyo, ni jukumu lenu kuandika habari zote mnazozipata hata kama tuhuma ilikuwa sio ya kweli, msikubali watu kupotosha wananchi kwamba ni jukumu lenu kuandika habari ambazo zimethibitishwa tu,
sio jukumu la wanahabari kuthibitisha tuhuma, wanahabari wanajukumu la kundika habari iliyo na pande mbili, sio jukumu la wanahabari kuficha baadhi ya HABARI baada ya mhusika kukanusha,

HII TUHUMA YA VYOMBO VYA HABARI WAONGO IPIGWE VITA
 
Back
Top Bottom