Vyombo vya dola mnakuwa wapi wakati uhalifu unatendwa?

Mama Mdogo

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2007
Posts
2,976
Reaction score
2,175
Ndani ya kipindi kisichozidi miaka 15, Tanzania kama taifa tumeshuhudia kwa kusikia na kuona matukio mengi kuhusu uhalifu na ufisadi mkubwa. Meremeta, Deep Green, Richmond, EPA, Escrow, container bandarini, rushwa wakati wa michskato ya uchaguzi, ubadhirifu Muhimbili etc.

Je kwanini kashifa hizi huwa haziibuliwi na vyombo vya dola mpaka vinavyohusu kazi hizo yaani TAKUKURU, POLISI na WIZARA HUSIKA. Ati ni mpaka wabunge au magazeti yaibue ndipo inatokea patashika ya kuziba hapa na pale.

Nafarijika kwa sasa haya mambo yanaibuliwa na viongozi wakuu (rais au waziri mkuu), lakini jee Takukuru, Polisi na Wizara husika wanafanya nini?
 
Duh! We unadhani Majaliwa alijuaje ile orodha ya Makontena yaliyoibiwa, mpaka kujua yote yalipitia geti no. 5?, magari yaliyotumika kubeba mzigo, wamiliki n.k kazi ya vyombo vya dola hivyo
 
Sasa ma Mdogo unafikiri hao wakuu na wabunge ndo wanafanya upelelezi? Hao wabunge viongozi wanasoma ripoti wanazopewa ambazo hazikufanyiwa kazi watakavyo
 
Duh! We unadhani Majaliwa alijuaje ile orodha ya Makontena yaliyoibiwa, mpaka kujua yote yalipitia geti no. 5?, magari yaliyotumika kubeba mzigo, wamiliki n.k kazi ya vyombo vya dola hivyo

Kazi ya chombo cha dola ni kukamata pale unapohisi kuna udanganyifu na si kusubiri Rais amalize madaraka yake aje mwingine ndio utoe madudu yaliyopita..
 
Umefundishwa wapi kuwa kazi pekee ya vyombo vya dola ni kukamata? Hata taarifa zote alizokuwa anasoma Majaliwa ni kazi ya vyombo vya dola. Kazi ya vyombo vya dola ni pamoja na kushauri Mamlaka ya juu na kutaarifu kwa wakati muafaka mambo kadhaa.
 
Nadhani kuna mahali hujamuelewa mtoa hoja. vyombo vya kama alivyo viainisha wajibu wao wa kwanza ni kuzuia uhalifu usitokee na kuwakamata wahusika na kuwafungulia mashitaka! sasa kama walikuwa wanajua kwanini hawakutimiza wajibu wao kama ambavyo huwa wanatimiza kuwakamata CDM na kuwapiga mabomu.kamatungepata Rais asiye jituma maana yake ni kwamba Nchi ingepata hasara. wewe unadhani makontena yote 349 yalitolewa siku moja? mengine huenda yalitolewa mwaka2009, 2010, 2013 muda wote huo wakakaa kimya basi nadhani kuna kasoro katika utendaji wao
 
Ndani ya kipindi kisichozidi miaka 15, Tanzania kama taifa tumeshuhudia kwa kusikia na kuona matukio mengi kuhusu uhalifu na ufisadi mkubwa. Meremeta, Deep Green, Richmond, EPA, Escrow, container bandarini, rushwa wakati wa michskato ya uchaguzi, ubadhirifu Muhimbili etc.

Je kwanini kashifa hizi huwa haziibuliwi na vyombo vya dola mpaka vinavyohusu kazi hizo yaani TAKUKURU, POLISI na WIZARA HUSIKA. Ati ni mpaka wabunge au magazeti yaibue ndipo inatokea patashika ya kuziba hapa na pale.

Nafarijika kwa sasa haya mambo yanaibuliwa na viongozi wakuu (rais au waziri mkuu), lakini jee Takukuru, Polisi na Wizara husika wanafanya nini?

Muda mwingi wanautumia kuhangaika na wapinzani na pia katika syllabus zao huwa wanafundishwa "Intelijensia" ya kupambana na upinzani tu na si vinginevyo huenda mitaala ibadilishwe
 
Back
Top Bottom