Vyeti vya kumaliza chuo Muhimbili

measkron

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
3,782
2,406
Madaktari na Madaktari Bingwa wanaomaliza mafunzo yao katika chuo cha sayansi ya tiba Muhimbili hawapatiwi vyeti vyao wakati wa Graduation tofauti na vyuo vingine vya Bugando na KCMC. Kwa sasa waliomaliza mwaka 2009 bado vyeti havijatoka wengune wamemaliza internship na kuajiriwa kwa utambulisho wa barua toka kwa Dean kwamba wamehitimu masomo yao na kutambulika kama madaktari na madaktari bingwa. Swali ni kwa nini vyeti visiandaliwe na kutolewa siku ya Graduation kama inavyofanyika Bugando na KCMC? kama kuna anayeweza kunipambanulia sababu humu jamvini naomba msaada.....nimepata kazi nje inayotaka cheti wakione na niwapatie kivuli cha cheti. sijaweza fanya hivyo. Shida ni uongozi wa chuo hauthamini wanafunzi kupata vyeti vyao kwa wakati?
 
Wanadai wanatengeneza vyeti Uingereza, ambako kuna kampuni inayowatengenezea pia UDSM. Vyeti hivyo ati hutumia angalau miezi tisa kutengenezwa. Na mara nyingi muda huongezeka wafanyakazi wa vyuo husika wanapochelewa kupitia upya usahihi wa taarifa zilizomo ndani ya vyeti.
 
Asante kwa taarifa,hii kitu hata mimi ilikuwa inanichanganya,.
 
ni kweli vyeti vya UDSM,Muh2 nadhani na chuo cha ardhi hutengezwa nje kuepuka kuchakachuliwa manake vingetengezwa bongo kila mtu mtaani angejiita daktari.nakumbuka nlisubiri mwaka ndio nikapata cheti cha kuhitimu digrii ya kwanza.sii mbaya kwa vile wanalinda kuchakachuliwa na wabongo wajanga manake hata mwaziri walidiriki kujiita madaktari wkt phd hawana mfano nchimbi na Kamala,pia Lukuvi na hadi leo hawajathubutu kumfungulia mashtaka yule bwana aliewatangaza hadhanrani kwenye kitabu chake wamefoji elimu.
 
.....mie nilimaliza 2009 pia sijapata,ila vitakuwa vimetoka nadhani maana inaelekea miaka 2 sasa. Nina mpango wa kwenda kuulizia june maana hapo nitakuwa nakihitaji haswa ili nitafute ajira.
 
Mkuu acha kabisa kutetea Uzembe na urasimu usio na maana kabisa, Ndio maana tuko nyuma kwa kila kitu, Inasikitisha na inakera saana, Kabla ya kutetea huu upuuzi ungejaribu kufanya kautafiti kidogo Vyuo vikubwa vya Kenya, Uganda, na Rwanda wanafunzi wanachukua muda gani kupata cheti,

Kwa taarifa yako Makerere chuo ambacho kina indani kubwa ya wanafunzi ukilinganisha na UDSM, Mhimbili na Ardhi wanafunzi wanapewa vyeti vyao siku ya mahafali. Na vyeti vyao wanachapishia nje pia, Hii imesaidia wanafunzi wengi kupata kazi kwa uharaka na waliotaka kuendelea na masomo kupata vyuo bila usumbufu

Kinachosikitisha kila kitu Tanzania tupo nyuma na wananchi tena tulioelimika tunatetea huu upuuzi,Naamini mtaamka Wakenya, Waganda na Warwanda watakapochukua kazi zote
 
.....mie nilimaliza 2009 pia sijapata,ila vitakuwa vimetoka nadhani maana inaelekea miaka 2 sasa. Nina mpango wa kwenda kuulizia june maana hapo nitakuwa nakihitaji haswa ili nitafute ajira.

Pole ndugu na mie nimemaliza Masters hapo Muhimbili 2009, kuna mtu kaenda kuangalia last week wamemjibu labda mwezi wa tano mwishoni. Undergraduate nimesoma chuo kikubwa zaidi ya mihimbili vyeti pia wanachapisha nje lakini niliweza kupokea cheti changu siku ya mahafali.
 
Hamna lolote la maana linalosababisha vyeti vichelewe kutoka zaidi ya urasimu uliokithiri kwenye vyuo vyetu.Siku hizi teknolojia ni kubwa hivyo haviwezi kuchelewa kama wana nia ya dhati.Mi nakumbuka tulichukua muda mrefu kupata hata academic transcript za MUCHS kisa eti gamba gumu la kuandikia hizo transcript lilikuwa limeisha! UCHENGE MTUPU!!!
 
Sijuhi kwa miaka ya hivi karibuni, lakini kwa kipindi cha nyuma hivyo vyeti vilikuwa vinaandikwa kwa Mkono, yaani kulikuwa na maandishi ya Komputa na sehemu za kujaza jina na degree uliyosomea huwa zinaandikwa kwa mkono kwa maandishi ya kuchonga ambayo hayapo kwenye komputer ili kuvifanya hivyo vyeti kuwa unique, sasa ukiangalia vyeti vya UDSM, Ardhi na MuSC vyote vilikuwa vinafanywa pamoja hivyo ni lazima vichukue muda sana kwani kila jina na degree uliyosomea inaandikwa kwa mkono, nina uhakika na ninalolisema, maana kuna jamaa yangu miaka ille cheti chake kilikuja na makosa kwenye jina na alipokwenda chuo kuomba kubadilishiwa aliambiwa atakipata baada ya mwaka kwani kitatumwa na wa hitimu wa mwaka unaofuata na sababu ni hizo nilizosema
 
Hakuna utetezi wowote hapa! Kushindwa kujiandaa ni kujiandaa kushindwa!

Kama unajua utolewaji wa vyeti nyako unachukuwa miezi mitatu basi Uongozi ujiandae kwa miezi mitatu kabla katika utaratibu wake wa masomo na masomo ili kulandana na siku ya mahafali.

Suala la mtu kuhudhuria mahafali (isipokuwa kama imetokea ajali fulani) bila cheti chake ni sawa na mtu kumaliza mwezi bila kupewa mshahara wake kwa kisingizio eti salary slip zimechelewa kutoka au sijui payroll bado hazijafika mkoani na upuuzi kama huo!

What if Mwanafunzi atatinga kwenye vipindi na kusema, "unajua anayenifadhili yuko ngámbo na ili kumuandaa mpaka kutuma fedha inachukua miezi sita au zaidi hivyo subirini karo lakini niendelee na shule."
Au Mfanyakazi alieajiriwa aseme, "Jamani itanichukuwa mpaka mwezi ujao ndio nianze rasmi lakini endeleeni kunilipa mshahara tu , tatizo ni kuwa bado hatujajipanga sawa na familia yangu na bado inanibidi nitoke kwanza honeymoon n.k"

Tabia hii inatakiwa ikomeshwe kabisa kila mahala. Unapodai chako uwe tayari kutoa chake kwa wakati muafaka!
 
Back
Top Bottom