samurai
JF-Expert Member
- Oct 16, 2010
- 11,495
- 24,212
Moja ya vitu vinavyosababisha hili taifa liendelee kukwama ni hili la VILAZ_A na VYETI FEKI.
kiukweli kwa hii speed ya Mh JPM nilitegemea sana hili suala ndio liwe la kwanza kufanyiwa kazi na kuliokoa taifa na mkwamo unaoletwa na hii jamii iliyojaa kwenye ngazi mbali mbali za kimaamuzi na utendaji.
Watu wasio na uwezo kiutendaji na wengine wengi wenye vyeti feki wamejazana sana kwenye mifumo mbalimbali ya taifa letu, hili ni suala muhimu kuanza kufanyiwa kazi kwa sasa maana kuendelea kufanya kazi ya kulijenga taifa hili huku ukiwa umezungukwa na jamii hii kiukweli kila kitu kitashindwa na kufa kabisa. Tanzania ya viwanda ni ngumu na haitawezekana huku tukiwategemea vilaz_a na watu wenye vyeti feki.
Vilaz_a wengi wameingia kwenye mifumo yetu kwa njia mbalimbali zisizo sahihi kwa maana ya kutofuata misingi ya ajira, njia hizo kwa mfano ni ngono,undugu,udini,rushwa,ukabila nk.
Ninapozungumzia vilaz_a namaanisha wale watu ambao hawana sifa na uwezo kiutendaji.
USHAURI;
Kuundwe bodi maalum itakayokula kiapo cha damu kufuatilia ajira zote za umma ikiwezekana hata kusaili watu upya ili kuwaondoa wale wote wasioweza kulisaidia taifa baadala yake wapo kusaidiwa na taifa kifupi wasio na uwezo na kustahili kuwepo sehemu husika. Uchunguzi ufanyike ili kujiridhisha kama kila mtu amepitia njia sahihi kupata ajira yake au kufika hapo alipo (promotion).kuwekwa misingi imara ili kupata kweli watu wenye uwezo kwenye mifumo yetu watakaoweza kushauri, kutenda na kuleta matokeo kwa manufaa ya taifa.
tuchangie na kuongeza nyama kwenye uzi labda wahusika wataona na kusikia kilio na hatimae kufanyia kazi.