Vyeti feki: Mabalozi, Wakuu wa Wilaya na Mikoa matumbo joto

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,945

Sakata la watumishi wa umma kushughi vyeti vya elimu limezidi kuchukua sura mpya na sasa wamefikia zaidi ya 10,000.

Hatua hiyo, inatokana na uhakiki uliofanywa na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ambayo imebaini waombaji kazi 39,511 kati yao, 1,951 wana vyeti vya kughushi.

Kuongezeka kwa idadi hiyo, kunatokana na kauli ya Rais Dk. John Magufuli, wiki iliyopita, kwamba anasubiri ripoti ya wafanyakazi wa Serikali ambao wamebainika kuwa na vyeti feki.

Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam, wakati akizindua mabweni mapya ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Alisema anafahamu idadi ya watumishi wenye vyeti feki ni zaidi ya 9,000 na anaisubiri ripoti hiyo kuifanyia kazi.

“Kwa hiyo mnaweza mkaona shida zilizopo katika nchi hii, huku wafanyakazi hewa karibu 19,000, wanafunzi hewa ni zaidi ya 56,000, kila mahali unapokwenda ni matatizo, lakini ni lazima niyatatue matatizo kwa sababu mlinichagua kwa ajili hiyo,” alisema Rais Magufuli.

Akiwasilisha hotuba ya bajeti ya mwaka 2017/18 kwa ofisi yake jana bungeni mjini hapa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki, alisema baada ya kubainika kwa hali hiyo, wahusika waliondolewa kwenye mchakato, huku vyeti hivyo vikiwasilishwa katika mamlaka husika kwa hatua za kisheria.

“Wahusika waliondolewa katika mchakato pamoja na vyeti hivyo kuchukuliwa na kuwasilishwa kwa mamlaka husika kwa ajili ya hatua zaidi,” alisema Kairuki.

Hata hivyo, zipo taarifa zinazodai kuwa orodha ya watumishi wa umma ambao wamebainika kuwa na vyeti feki itawekwa hadharani Aprili 30.

Zaidi inaelezwa kuwa sakata hilo la vyeti feki linawagusa
Mabalozi ambao ni wawakilishi wa Tanzania katika mataifa mbalimbali,Wakuu wa wilaya na Wakuu wa Mikoa
 
Sakata la vyeti feki hatimae idadi imefikia 10000, kati yao wapo mabalozi, Wakuu wa wilaya na wakuu wa Mikoa
Kwa kuwa hao ni wateule wa Rais tunajua Rais atawaondoa mara moja katika nafasi zao ili waingie katika mikono ya sheria
Mh Rais amekua akipiga vita sana vyeti feki kwa watumishi wa serikali/ umma hata kufikia hatua ya kusema hatakua na msalie mtume kwa wenye vyeti feki, kwa maana hiyo baadhi ya wakuu wa wilaya, mikoa na mabalozi sasa wapo katika wakati mgumu sana kufuatia kauli ya Mh Rais kuhusu tuhuma hizo.
Si kweli penye red, acha unafiki, sema ukweli na utakuweka huru! the man has never been serious,
 
Back
Top Bottom