Al-Watan
JF-Expert Member
- Apr 16, 2009
- 11,891
- 14,563
Sina shida na uhakiki wa vyeti. Nina tatizo na zoezi kufanywa kiholela, watu kutopewa nafasi ya kujieleza na kukata rufaa kabla majina hajayachapishwa, upuuzi wa kina Bashite kuachiwa na maigizo ya serikali kutaka sifa ionekane inafanya kazi zaidi ya kutaka kutatua tatizo.Wewe utabaki na kelele tu Serikali haina umakini inakurupuka basi.Wewe ulikuwa unajua kuwa kuna watu wanatumia vyeti fake na umewahi kupiga kelele yoyote??? Sasa hivi wanaume wanaongea na kuchukua hatua na wengine mnaanza kupiga kelele zisizokuwa na msingi wowote!!
Na hii ni awamu ya kwanza awamu ya pili inakuja pia itakayohusu wizara na na mashirika ya umma nao wajiandae tu.
Tatizo letu tumeuziwa vyetu tumenunua na kuombea kazi au kuchomeka ktk mafaili kazini umekuja uhakiki imegundua ni cheti fake.
Wengine hata Chuo alichosoma hajui details zake au shule aliyosoma haijui kabisa ila ameng'ang'ana tu nimesoma Kibasila Secondary lakini hata haijui iko wapi...maajabu kabisa na cheti chenye si chake
Kanuni moja kubwa sana ya uongozi bora ni kwamba, kiongozi hatakiwi kuwataka walio chini yake wafanye kitu ambacho yeye hawezi au hataki kufanya.
Yani ni kwamba, kama kamanda wa jeshi anawataka walio chini yake wapige mbizi kuvuka mto, yeye mwenyewe anatakiwa kuwa mfano kwa kuanza kupiga mbizi na kuwaita wengine wamfuatilie.
Asije kuwaambia wenzake wapige mbizi katika mto ambao hakuna mtu anaweza kuuvuka.
Sasa kwa nini katika zoezi hili tunaletewa ujinga wa double standard, watu fulani wanahakikiwa, kina Bashite wanaachiwa?
Wewe unaona upumbavu huu sawa?