barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Mara ya kwanza kumfahamu ni miaka kadhaa iliyopita,ambapo ndugu na jamaa yangu wa karibu alipata ajali eneo la Doma Morogoro na kwenda kufia katika hospital ya mkoa wa Morogoro.
Wakati huo,bila ya shaka na kwa uhakika wa karibu,Daktari Mkuu wa Hospital ya Mkoa alikuwa Mahizo.Alituhudumia kwa upole na ukarimu.Mjuzi na mweledi katika fani yake,akitoa ushauri wa kitaalam na hatimaye kutupatia rufaa kwa baadhi ya majeruhi kufika Muhimbili.
Baadae akawa jamaa na rafiki wa hapa na pale sbb ya msaada na majitoleo yake kwa siku ile.Ndipo nilipofahamu kupitia yeye na marafiki zake kuwa amesoma Urusi.Ni daktari mbobezi na mweledi katika fani yake.Huyu alipasua na kutahiri,alipima na kuandika dawa.Ni dokta kwelikweli aliyevuka mipaka mpaka Ulaya ya Mashariki kuitafuta elimu.Msomi wa Urusi,ile Urusi ya Kisoviet ya Mwalimu Nyerere
Sasa naliona jina lake no4972 katika mtiririko wa majina matatu kama mmoja ya wenye "vyeti feki".Najiuliza kwa kunong'ona,huyu aliwezaje kufika chuo?Ilikuwaje mpaka alivuka mipaka,akasoma na kufaulu kwa "cheti feki?"Ilikuwaje akapata madaraka makubwa kwa ngazi ya kada yake bila kujulikana?Iweje akawa "bingwa"?akapasua na kutahiri bila "cheti orijino?"
Mwaka huu alikuwa astaafu na aendelee na mambo yake,fagio la JPM limemkumba.Najiuliza iliwezekanaje mpaka kufikia huko juu bila kugundulika?Hili la vyeti limetushangaza wengi,lkn limetufunza pia...