Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
1920-30 - Julius Nyerere, George Kahama, Rashid Kawawa
1930-40 - Cleopa Msuya, John Malecela, Benjamin Mkapa
1940-50 - Anna Makinda, Joseph Warioba, Jakaya Kikwete
1950-60 - Benard Membe, John Magufuli, Samia Suluhu Hassan
1960-70 - Lazaro Nyalandu, Stella Manyanya, Hussein Mwinyi
1970-80 - January Makamba, Emmanuel Nchimbi,Mwigulu Nchemba
Hivyo ni vizazi sita vya uongozi wa juu wa CCM. Mimi sio mwanahistoria, ninachotaka kukiongelea ni jinsi gani kizazi kimoja kinavyoweza kurithisha uzoefu wa kisiasa kwa kile kinachofuatia (succession plan). Vyama vingi sana barani Afrika hukosa hiyo tabia ya kurithishana uzoefu, matokeo yake ni mvurugano usiokuwa na mwisho (political chaos).
Tunaposikia kuwa vyama kama Republican, Democrat, Labour na Conservative, vina miaka mingi tangu vianzishwe, kinachokuwa kimefanyika katika kuutunza uhai mrefu wa chama ni ule uwezo wa kizazi kimoja kugawa uzoefu kwa kile kinachofuata. Kizazi cha Nyerere kiliwapokea kisiasa kine Msuya. Kizazi cha kina Msuya kiliwaongoza kisiasa kina Makinda. Kizazi cha kina Makinda kiliwaongoza kina Membe. Kizazi cha kina Membe ni waalimu wa kina Nyalandu. Kizazi cha kina Nyalandu kiliwaongoza kina Nchimbi, na wao hivyo hivyo wakawafundisha siasa wadogo zao waliozaliwa kwenye miaka ya 90.
Bila ya kuwepo kwa succession plan inayoeleweka, vyama vya siasa mara nyingi hubakia kuwa ni kundi fulani la wajuaji, ambalo kifo chake hakipo mbali, yaani uhai wake ni mfupi kwani misingi na imani ya chama, vinakuwa ni vitu viwili ambayo havina waalimu wa kuvirithisha.
Navitakia vyama vyote vya siasa nchini, ule uwezo wa kujenga tabia ya kurithisha uzoefu kutoka kizazi kimoja kwenda kingine, ili malengo mapana ya uanzishwaji wa vyama yaweze kueleweka kutoka kizazi kimoja kwenda kingine. Na matokeo yake ni vyama vya siasa kuweza kuwa na uhai mrefu ambao utachangia katika kukomaza tamaduni mbalimbali za kisiasa.
Haya ni mawazo yangu, waungwana siku njema.