Vyama vyaanza kunyemelea Arumeru Mashariki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vyama vyaanza kunyemelea Arumeru Mashariki

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by MziziMkavu, Feb 13, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 13, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Vyama vya upinzani vimejiandaa kukikabili Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi wa Jimbo la Arumeru Mashariki mkoani Arusha ambapo vimetuma wanachama na viongozi wao kwenda kufanya kufanya utafiti kuhusu hali ya kisiasa ilivyo kabla ya kutangaza kuweka wagombea wao.Uchaguzi katika jimbo hilo unafanyika kufuatia aliyekuwa mbunge wake, Jeremiah Sumari (CCM) kufariki dunia. Kampeni zitaanza Machi 9, mwaka huu na kufuatiwa na uchaguzi Aprili Mosi, mwaka huu.Naibu Katibu Mkuu wa CUF,Julias Mtatiro, alisema chama chake kimetuma watu kupeleleza jimboni humo na baada ya hapo itatolewa taarifa rasmi ya chama kuhusu msimamo.“Chama kitatoa tamko rasmi kuhusu msimamo wa chama na Jumapili wiki hii, lakini kwa sasa wapo watu tumewatuma wanafanya tathmini jimboni humo kuangalia hali ilivyo,” alisema Mtatiro.Mwenyekiti wa TLP, Agustino Mrema, alisema chama chake kitasimamisha mgombea katika jimbo hilo kwa sababu kina historia nzuri katika jimbo la Arumeru Mashariki. Alisema histori nzuri ya chama hicho inatokana na kufanikiwa kusuluhisha mgogoro mkubwa baada ya watu walichoma moto Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), nyumba na watu kadhaa kuuawa.Katibu wake Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Samweli Ruhuza, alisema chama kimetuma watu ambao wamekwenda jimbo humo kuangalia hali ilivyo kabla ya kutoa uamuzi wa mwisho wa kuweka mgombea wao kuchuana na wagombea wa vyama vingine.Mkurugenzi wa Habari wa Chadema, John Mnyika, alisema chame chake kitatoa taarifa rasmi leo kuhusu ushiriki wake kuhusu uchaguzi huo.CHANZO: NIPASHE
   
 2. N

  NDOFU JF-Expert Member

  #2
  Feb 13, 2012
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 656
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Chama cha kijamii vp?..INAIDI KIENDE NACHO KIKAONESHE UWEZO WAKE WA KUNADI SERA.
   
 3. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #3
  Feb 13, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Chadema tunalichukua jimbo....
   
 4. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #4
  Feb 13, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Nimesikia mtoto wa Marehemu ameamua kugombea kiti alichoacha baba yake!!
   
Loading...