Vyama vya wafanyakazi vipo wapi?

famousrkr

JF-Expert Member
Feb 6, 2013
295
228
Leo hii wale wa wanufaika wa bodi ya mkopo ya elimu ya juu (HESLB) wameonja joto la jiwe baada ya kukukuta makato ya 15% kwenye mishahara yao.

Kulipa deni sio vibaya lakini ni namna gani unalipa deni ikiwamo makubaliano mliyokubaliana na mdeni wako.

Inakuwaje HESLB wavunje makubaliano ya 8%?, vile vile wanafikiliaje wadeni wao jinsi watakavyoishi?

Je, vyama vya wafanyakazi kama vile CWT, TUGHE,TALGWU et al mko wapi wateja wenu wanalia?
 
Hivyo vyama uliwahi visikia tangu kuanza kwa 'ngwe' hii?
Imebakia kuvaa fulana za vyama hivyo tu ila sina hakika na role yao kama inaonekana. ...
 
Wafanyakazi TZ hawana vyama
Jumuia ya ccm wakuu wa vitengo vyake wakaanzisha vyama na kuagiza waajiriwa wajiunge ati ndiyo vyama vya kisekta. Siku wafanyakazi wakuanzisha vyama vyao mahali pa kazi na kuungana kadri ya mfanano wa sekta na malengo ndipo kutakuwa na Tija.
Kwa sasa poleni
 
Hivi vyama vyote vimekua hoi hoi hakuna
Chama cha wafanya kazi
Cha wafanya biashara
Cha viwanda ..wote kimyaaaa...
 
Wala usitegemee vyama hivyo vikutetee... Viongozi wa vyama hivyo wako kwenye payroll ya anayekudai!!!
 
Kama kuchelewa mulishachelewa, kipindi sheria inafanyiwa marekebisho hamukuliona hili mkapiga kelele? Kwa uongozi huu wa kufuata sheria zinazoonekana zinaongeza mapato,tusahau kabisa. Kelele inatakiwa toka mwanzo wa kutunga sheria. Angalia walivomsakama Makonda kisa kawagusa. Hili la 15% na Fao la kujitoa hawakuyaona na sisi tulivo
watu wa ajabu hatuoni kwa nini wenzetu wanaungana kutetea matumbo yao
 
Back
Top Bottom