Vyama vya siasa vyatakiwa Kurejesha Gharama za Uchaguzi kwa mwaka 2015

Kagondo

JF-Expert Member
Jun 6, 2016
296
79
IMG_20160622_134458 (3).JPG

Vyama vya siasa nchini, vilivyohusika katika harakati za uchaguzi mkuu 2015, vyatakiwa kurejesha ripoti ya gharama zilizotumika kuanzia kampeni hadi siku ya mwisho ya uchaguzi.

Sheria ya gharama za uchaguzi Namba 6/2010, inawataka wagombea wa vyama vyote kwa ngazi za Udiwani, Ubunge na Urais, kuwasilisha ripoti ya gharama walizotumia kwa vyama vyao ndani ya siku tisini (90) baada ya siku ya kupiga kura, hii ni bila kujali kama ameshinda au kushindwa katika nafasi aliyokuwa anawania.

Pia, kila chama cha siasa ambacho kimedhamini mgombea, kinatakiwa kuwasilisha ripoti kwa msajili iliyotoka kwa mgombea/wagombea ikiwa na marejesho sahihi katika fomu maalum ambayo inaonesha stakabadhi zote na risiti za gharama zilizotumika.

Haya yameelezwa leo na Msajili msaidizi gharama za uchaguzi na Elimu kwa umma, Bi. Piencia Kiure kwa waandishi wa habari waliofika ofisini kwake, ambapo amebainisha kuwa, vyama viwili pekee ndivyo vimerejesha ambavyo ni ACT na CCM kilichorejesha leo.

Pia, ametoa wito kwa vyama vingine kuwasilisha marejesho hayo kabla ya tarehe 25 mwezi huu, na kutahadharisha kuwa, faini itatolewa pamoja na adhabu kwa vyama vitakavyokiuka kutekeleza agizo hilo kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi inavyoeleza.

Faini hiyo ni kulipa shilingi milioni tatu (3) pamoja na kujipotezea sifa za kushiriki uchaguzi wowote ule, ikiwemo uchaguzi mkuu utakaofuata, isipokuwa tu kama chama kitawasilisha ripoti ya fedha na ukaguzi kwa namna itakayomridhisha Msajili kabla ya siku ya uteuzi itakayopangwa.
 
sheria za ajabu hizi, hazina impact yoyote katika maendeleo na kukuza demokrasia, sheria kama hizi hufanya kazi pale tu watawala wanapotaka kuwabana wapinzani
 
sheria za kijinga jinga hizi, hazina impact yoyote katika maendeleo na kukuza demolrasia, sheria kama hizi hufanya kazi pale tu watawala wanapotaka kuwabana wapinzani
Kwikwikwiwkiw.
 
Ngoja tuone marejesho ya mahesabu ya muunganiko wa vyama vya upinzani. Lazima wachelewe kidogo..ili kufanya yao kabla ya kupeleka mahesabu.
 
sheria za kijinga jinga hizi, hazina impact yoyote katika maendeleo na kukuza demolrasia, sheria kama hizi hufanya kazi pale tu watawala wanapotaka kuwabana wapinzani
Transparency ni moja ya elements za good governance, kwahiyo vyama vinatakiwa kuwa na uwazi wa mapato na matumizi yao, isijekua tunaruhusu watu hatari kushika dola, kama hawana elements za uwazi toka mwanzo.
 
Back
Top Bottom