Vyama vya siasa vyaaswa kushiriki Uchaguzi wa Zanzibar

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Mhe.Jaji Francis Mutungi ameviasa Vyama vya Siasa kushiriki chaguzi zinazotangazwa na tume za uchaguzi nchini ikiwemo uchaguzi wa Machi 20, mwaka 2016 uliotangzwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

Kwa mujibu wa barua iliyotolewa kwa vyama hivyo leo na kusainiwa na Jaji Mutungi ilieleza kwamba, kimsingi Sheria ya Vyama Vya Siasa Sura ya 258 inasisitiza vyama vya siasa kushiriki katika chaguzi zote zinazotangazwa na tume za uchaguzi ili kufikia malengo yake ya kushika dola.

“Katika nchi kidemokrasia na kwa chama cha siasa kinachoamini misingi ya kidemorasia ya vyama vingi vya siasa, hakuna njia mbadala kwa chama cha siasa kufikia malengo yake zaidi ya kushiriki uchaguzi.

“Ni wajibu wa kila chama cha siasa nchini kama wakala wa kukuza demokrasia, utawala wa sheria na amani ya nchi, kuwa wa kwanza kutii matamko ya kisheria yanayotolewa na mamlaka husika .

Kama kuna chama cha siasa hakiridhiki au kimekwazwa kwa njia moja au nyingine na suala lolote kuhusu masuala ya uchaguzi, njia stahiki na inayonyesha ukomavu wa kisiasa si kuhamasisha kugomea uchaguzi, bali ni vema kikafuata utaratibu uliowekwa katika sheria za uchaguzi,” alisema Jaji Mutungi.

Aidha Msajili huyo amesema kwa mujibu wa Sheria za Nchi bado ni suala la hiari kwa chama kushiriki uchaguzi lakini utashi huo wa hiari unaenda sanjari na umuhimu wa kila chama kushiriki kila uchaguzi unaotangazwa na tume ya uchaguzi.

“Hivyo ni muhimu basi kila chama cha siasa kuelewa kuwa,uchaguzi ni kipimo cha uhai wa chama cha siasa. Chama cha siasa kisiposhiriki uchaguzi kinaua uhai wake katika mtazamo wa harakati za kisiasa,” alisisitiza.

Aliongeza kwamba hivi sasa, mfumo wa demokrasia ya vyama vingi na vyama vya siasa vimeimarika, hivyo sio vyema kwa chama cha siasa kujirudisha nyuma au kujiua kisiasa kwa kutoshiriki uchaguzi wakati kina uwezo wa kufanya hivyo.
 
12472266_1030012200396571_5627849878258240193_n.jpg
 
Hivi huyu msajili ametumwa? Inawezekaje ukawa unashiriki uchaguzi huku mpinzani wako anayetawala haonyeshi dalili ya kutoka madarakani hata kama ameshindwa.huyu msajili angekuwa ni muungwana kama angekemea kauli za kibaguzi zinazotolewa na ccm sio kuja na pumba zake hapa.
 
Habari za Zanzibar hazina mvuto tena, watu wanaona bora kujadili gwanda alilovaa Rais au kuoneshwa 'live' bunge.
Sijajua ningekuwa natokea huko ningeuchukuliaje muungano.
 
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Mhe.Jaji Francis Mutungi ameviasa Vyama vya Siasa kushiriki chaguzi zinazotangazwa na tume za uchaguzi nchini ikiwemo uchaguzi wa Machi 20, mwaka 2016 uliotangzwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

Kwa mujibu wa barua iliyotolewa kwa vyama hivyo leo na kusainiwa na Jaji Mutungi ilieleza kwamba, kimsingi Sheria ya Vyama Vya Siasa Sura ya 258 inasisitiza vyama vya siasa kushiriki katika chaguzi zote zinazotangazwa na tume za uchaguzi ili kufikia malengo yake ya kushika dola.

“Katika nchi kidemokrasia na kwa chama cha siasa kinachoamini misingi ya kidemorasia ya vyama vingi vya siasa, hakuna njia mbadala kwa chama cha siasa kufikia malengo yake zaidi ya kushiriki uchaguzi.

“Ni wajibu wa kila chama cha siasa nchini kama wakala wa kukuza demokrasia, utawala wa sheria na amani ya nchi, kuwa wa kwanza kutii matamko ya kisheria yanayotolewa na mamlaka husika .

Kama kuna chama cha siasa hakiridhiki au kimekwazwa kwa njia moja au nyingine na suala lolote kuhusu masuala ya uchaguzi, njia stahiki na inayonyesha ukomavu wa kisiasa si kuhamasisha kugomea uchaguzi, bali ni vema kikafuata utaratibu uliowekwa katika sheria za uchaguzi,” alisema Jaji Mutungi.

Aidha Msajili huyo amesema kwa mujibu wa Sheria za Nchi bado ni suala la hiari kwa chama kushiriki uchaguzi lakini utashi huo wa hiari unaenda sanjari na umuhimu wa kila chama kushiriki kila uchaguzi unaotangazwa na tume ya uchaguzi.

“Hivyo ni muhimu basi kila chama cha siasa kuelewa kuwa,uchaguzi ni kipimo cha uhai wa chama cha siasa. Chama cha siasa kisiposhiriki uchaguzi kinaua uhai wake katika mtazamo wa harakati za kisiasa,” alisisitiza.

Aliongeza kwamba hivi sasa, mfumo wa demokrasia ya vyama vingi na vyama vya siasa vimeimarika, hivyo sio vyema kwa chama cha siasa kujirudisha nyuma au kujiua kisiasa kwa kutoshiriki uchaguzi wakati kina uwezo wa kufanya hivyo.
HIVI Hawa Ndio Wale MAJAJI Ambao Aliwahi Kusemwa Na Mh. Tundu Lissu Bungeni, Kuwa WAMETEULIWA Tu, ILI Mradi Kujaza Namba!!!!??? KAMA Amesema Ni Kwa Mujibu Wa SHERIA Ya VYAMA Vya SIASA NCHINI!!! NA Ni Vyema VYAMA Vya SIASA Kutii Matamko / Matangazo Ya TUME YALIOTANGAZWA Kwa Mujibu Wa SHERIA Zake Na Zile Za UCHAGUZI!!!! HAPO Ndipo Penye Msingi Wa Swali Langu!!!! HIVI Kwa Mwanasheria Wa Kiwango Cha JAJI, ANASHINDWA Kujua Kuwa Kwa Mujibu Wa SHERIA Za UCHAGUZI ZANZIBAR, TUME (ZEC) Haingiliwi Ktk. Maamuzi Yake Na Hauwezi Kwenda MAHAKAMANI KUHOJI Maamuzi Yake!!!?? NDIO Maana WANASHERIA Wameshindwa Kwenda MAHAKAMANI KUPINGA Tangazo La JECHA La KUFUTA MATOKEO Ya UCHAGUZI Wa 25Oct 15 Na Hili La Kutangaza Tarehe Ya UCHAGUZI Wa Marudio!!! Ingawa Wameona Na Kujua, Kuwa Matangazo Na Maamuzi Yote Hayo. Yamekiuka Sheria Na Katiba!!! NDIO Maana JECHA AMESHINDWA Kutaja Kifungu Chochote Cha SHERIA Za ZEC, UCHAGUZI Au KATIBA Ya ZANZIBAR Kinachompa Mamlaka Ya Kufanya Yale!! PIA Kushiriki UCHAGUZI Wowote Ni Hiari Kwa Chochote Cha Siasa!!!! SASA Yeye Kama JAJI AMESHINDWA Kuona Faida Na Hasara Ya CUF Kushiriki UCHAGUZI Huo BATILI!!!? Ni BORA CUF Kifutik
 
Sijui kwa nini wasomi wa Tanzania wanaweka elimu zao mfukoni kisa hayo matumbo sasa na huyu ni jaji kweli anazungumza nonsense
 
Maeneo hayo yana ashiria nini kwa Taaluma aliyokuwa nayo Msajili. Akili kaacha mfukoni au upeo wake mdogo? Hajui lengo kuu la chama chochote cha Siasa ni Kushika Dola. Na kama watawala hawataki kukabidhi dola unashiriki kwenye uchaguzi lengo liwe nini? Kushiriki au kusindikiza. CCM kuna wanataaluma tena magumashi na sio wasomi
 
Back
Top Bottom