Wakati watumishi wa vyama vya upinzani na asasi mbalimbali za kiraia zilipigwa marufuku kujumlisha, kutangaza, na kutunza rekodi za matokeo ya uchaguzi wa wabunge na urais mwaka 2015, vyama vya siasa, waandishi wa habari, na asasi za kiraia zimeruhusiwa kuwa na vituo vya kukusanya, kumjumlisha na kuhifadhi kumbukumbu ya matokeo ya kura katika uchaguzi mkuu ujao nchini Kenya. Nini maoni yako kwa uamuzi huu wa majirani wetu Kenya? Na Je, Serikali ya Tanzania inaweza kuruhusu jambo hili kwa uchaguzi wa mwaka 2020 ili kuondoa tuhuma za chama tawala kuchakachua kura?