Vyama vipya vya kisiasa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vyama vipya vya kisiasa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kadogoo, Jan 23, 2011.

 1. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #1
  Jan 23, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ni miaka 50 sasa tangu tumepata uhuru lakini bado umaskini, ujinga, maradhi na sasa ufisadi vinatuzungukia na kutunyima usingizi!

  Vyama vyenye mrengo wa ki-secular ndivyo vimetufikisha hapa tulipo! sasa nadhani umefika wakati Katiba mpya iruhusu vyama vingi vikiwemo vyama vyenye muelekeo wa kidini ili kupanua demokrasia zaidi kwani huko tulikoiga hiyo demokrasia hasa nchi za Magharibi tumeona vyama kama Cristian Demokratic Party huko ujerumani, Cristian party huko Norwey, nk, waliunda Serikali na nchi zao zimepiga maendeleo makubwa sana ya kiuchumi, kisiasa, kijamii nk!

  Watanzania ,kauli ya kuchanganya Dini na Siasa ni uhaini! imepitwa na wakati natumai Katiba yetu mpya itaruhusu pia wananchi wanaotaka kuchangia maendeleo katika nchi yao kuanzisha vyama vyenye mrengo wa mafundisho ya kiroho maana roho na mwili vinaenda sambamba!

  sio haki kabisa kuwaachia baadhi ya Wanachi wasioamini dini waendelee kuongoza nchi peke yao huku siasa zao za Ki-secular zimeshindwa kuwatoa WaTanzania katika dimwi la ufukara! huu ni wakati muafaka wa kuwajaribu na wenzetu Waumini wa Dini nao waanzishe vyama vya kisiasa ili uchaguzi ujao tupate kuchagua chama tunachoona kinafaa kuongoza nchi yetu!

  Tunaomba wasioamini dini wawavumilie wenye dini! hii ndio DEMOKRASIA!
   
 2. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wazo zuri, kwa kuanzia mimi na shauri Wakristo chao kiitwe CRISTIAN DEMOKRATIC MOVENMENT na cha Waislamu kiitwe TANZANIA ISLAMIC PARTY! na wengine kama Hindus na wasio na dini nao wanaweza kuanzisha ila sishauri vyama vya kikabila! TZ tuna makabila mengi sana hivyo kama kila kabila likianzisha lake tutakuwa na utitiri wa vyama!
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Jan 23, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  WATANZANIA NI WANGAPI HADI SASA (2005 - 2010) WENYE MAISHA BORA NA HADI HIVI SASA (2010 -2015) WAO WANAJIBIDISHA TU KUTAFUTA KIADA CHAKE NCHINI????

  Watanzania wenzangu tuambizane ukweli hapa na tusifichane hali halisi ndani ya mifuko yetu. Mpaka hivi sasa wengi wetu HATUZUNGUMZII TENAUCHUMI wa maisha yetuTanzania bali hali halisi ni UCHUMA wa maisha yetu nchini. Je, wewe????

  Baya zaidi, ajabu ninayoiona nkule bado CCM na JOPO LA MAFISADI wangependa Watanzania wote tukaseme tu YOTE NI MAISHA na kukimbilia kitanndani, baada kucheka na Masanja TBC, huku CC ya CCM wakibariki Dowans walimpwe.

  Huku waliosbobea katika uchumi nchini wanatutahadharisha KIAMA DOWANS WAKILIPWA na kuongeza kuongeza kwamba tunachoona mpaka sasa kwa gharama ya maisha eti hapo bado ni mwanzo tu wa mapinduzi ya sinema nzima wa ahadi ya Maisha BORA ZAIDI kwa kila Mtanzania; na katika kutimiza hilo Mhe Kikwete na CCM wametuhakikishia dhamira zao za kutufikisha huko kwa Nguvu Zaidi, Ari Zaidi na Kasi Zaidi.

  Sasa Mtu endapo utakuwa hauoni MAISHA BORA ZAIDI basi wala usisubiri kuambiwa na mtu, Wenye kuona UGUMU ZAIDI KWA KILA NAFSI YAKE huyu si Mtanzania tena maana WATANZANIA WOTE waliopata ahadi hizo tangu siku nyingi tu (2005 - 2010) maisha yao ni bora kabisa hivi sasa (2010 - 2015) wanacho kitafu kiukweli ni Uziada wa UBORA HUO WA MAISHA.
  HOJA YANGU:

  Kwa mantki hiyo Mhe Kikwete na CCM, watu wa Takwimu nchini acheni kutu fikicha ukweli, Watanzania ni wastani wa watu wangapi nchini maana hili la watu milioni 46 wala sihitaji tafsiri ya mtaalamu kubani kwamba si kweli.
   
 4. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #4
  Jan 23, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Rudi katika mada!
   
 5. d

  dos santos JF-Expert Member

  #5
  Jan 23, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 240
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  kuna watu wanaingia jamvini tayari washapiga mbege mtu anazungumzia mada hii yeye anazungumzia kitu kingine. Pumbaf tatizo ni kukaririshwa hoja
   
 6. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #6
  Jan 23, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Usijali, hakuna kulala mpaka kieleweke!
   
 7. T

  Topical JF-Expert Member

  #7
  Jan 23, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  I predict thats no longer unavoidable, if you have a priest who wants to be a president then it becomes relevant for sheikh to become a president

  Hilo kwa sasa liko wazi nashukuru naombea lije haraka
   
Loading...