Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,132
- 10,514
Kwa muda mrefu sasa, jina la Jose Mla Vichwa limekuwa gumzo mitaani, mitandaoni na hata meza za chai za ofisi nyingi hapa nchini. Ni mtu anayeonekana tofauti, mtu mwenye hamu ya kugusa, kuonja na kula vyakula ambavyo Watanzania wengi hawaitaji hata kuvisikia.
Kicheche, kenge, panya, chatu – kwa Jose hivi ni kama nyama ya kawaida ya ng'ombe, mbuzi au kuku. Huu ni upande wake wa kipekee, ambao mara nyingi huacha mashabiki wake wakibaki na mshangao, huku wengine wakimuona kama mtu wa hatari anayejaribu kutikisa misingi ya utamaduni wa chakula cha Kitanzania na Kiafrika.
Lakini je, safari hii Jose anaelekea mbali zaidi ya utamaduni na kuingia kwenye eneo hatarishi la maisha yake?
Wataalamu wa afya wanabainisha wazi kuwa si kila mnyama anayekula nyama unaweza pia kumla wewe. Kuna wanyama wenye sumu kali sana, ambao ukijaribu kugeuza kitoweo, basi kitakuwa ndio tiketi yako ya moja kwa moja kwenda kaburini.
Moja ya mifano hai ni samaki maarufu Pufferfish (Fugu), anayejulikana sana duniani. Ni chakula cha kifahari kinachohitaji mpishi mtaalamu mwenye leseni maalumu. Kosa dogo tu katika maandalizi yake, na nyama ya samaki huyu hugeuka sumu kali sana. Hata Jose mwenye tumbo la chuma asithubutu kupima hatari hii.
Kisha kuna Blue-ringed Octopus, kapweza kadogo kwa umbo lakini kajamaa kana sumu kali inayoweza kuua mtu mzima ndani ya dakika chache. Wakati watanzania wengi tunafurahia mchuzi wa pweza, na ubora wake katika kuhimarisha nguvu za kiume, Kaka Jose asije akajikuta amechanganya bakuli na kachori zako utajikuta kwenye wakati mgumu sana.
Hali ni hiyo hiyo kwa Cane Toad, chura mkubwa ambaye ngozi yake inatoa sumu ya aina ya bufotoxin. Wengine wamejaribu kumla na ugali maharage lakini matokeo yake mara nyingi ni vifo visivyotarajiwa.
Kwa mtindo huu wa kula vyakula visivyo vya kawaida, Jose anachochea mjadala mpana kuhusu usalama wa chakula na utamaduni wa Tanzania. Je, tunaposhabikia upekee wake, tunasahau kuwa kuna mpaka kati ya kula chakula cha kienyeji na kula sumu kwa makusudi?
Hata wageni ambao unawapatia mwaliko mara kadhaa, kuwa makini maana mgeni anaweza kutamani kuonja nyama ya Kuku Makucha, kumbe ana allergy, kinamlamba vizuri kabsa. Wakija wageni wako wape tahadhari mapema na kama inawezekana wape chakula cha kawaida. Sio kila mtu umpatie nyama ya Kuku Makucha.
Ila yote kwa yote Kaka Jose, endelea kuwa mbunifu, lakini kumbuka: hamu isije ikawa adui wa maisha.