Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,618
- 9,609
BAADHI YA VYAKULA VYA KUONGEZA DAMU MWILINI NI PAMOJA NA;
1. Baadhi ya matunda husaidia kwa kiwango kikubwa katika kuongeza damu mwilini, na matunda hayo ni pamoja na; Matunda Damu, Zabibu, machungwa, maembe,nyanya pamoja na Strawberries.
2. Ulaji wa mbogamboga kama vile matembele,Spinach au Sukuma wiki pia husaidia kwa kiwango kikubwa kuongeza damu. Pendelea kula mboga mboga hasa hasa mboga jamii ya matembele zitakusaidia sana kuongeza wingi wa damu mwilini.
3. Pendelea kula vyakula vywenye vyanzo vizuri vya Madini aina ya Chuma Kama vile; maharage,nyama au maini.
4. Matumizi ya juisi mbali mbali kama juisi ya Rozella,Tikiti maji, karoti au nyanya huongeza Damu kwa kasi sana. Hivo pendelea kutumia aina hizi za Juisi.
5. Zipo njia nyingine za kuongeza Damu katika mwili wa Binadamu kama vile; matumizi ya Dawa aina ya FEFOL ambapo hapa kuna kiwango kikubwa cha madini ya chuma ambayo yatasaidia utengenezwaji wa haraka wa damu,na hivo kuongeza kiwango cha damu mwilini.
Endapo Mgonjwa yupo katika hali ya hatari ya kuishiwa na damu,zipo njia za haraka kama kutundikiwa damu moja kwa moja kwa njia ya Drip.