Vurugu Zanzibar, matokeo ya udini au Uchaguzi Mkuu 2010? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vurugu Zanzibar, matokeo ya udini au Uchaguzi Mkuu 2010?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dosama, Jun 3, 2012.

 1. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Na Deogratius Temba, Tanzania Daima

  PENGINE tunaweza kupingana, kukosoana na kutokukubaliana kuwa tatizo au sababu ya vurugu za Zanzibar zilizotokea wiki iliyopita ni udini au chuki za kiimani zilizoasisiwa na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati wa uchaguzi Mkuu mwaka 2010. Tuna kila sababu ya kuendelea kuwalaumu na kuwalaani wanasiasa waliotufikisha hapa.

  Hali ya hewa imechafuka wao wamekaa pembeni! Hata kama Muungano utavunjika ni kwa uzembe wao. Haya ni matunda ya kutumia udini kujinufaisha kisiasa, walifanikiwa kuwagawa Watanzania kimakundi, ili wawatawale kirahisi.

  Hii ilikuwa ni mbinu ya chama tawala kulikuza suala hili, wakilitumia kama mbinu ya kuua au kudhoofisha upinzani baada ya ukabila kushindwa.

  Sababu nyingine ya CCM na viongozi wake kupandikiza mbegu ya udini ni kutaka kuvunja nguvu ya upinzani, baada ya kuona CHADEMA inakuja kwa kasi hasa baada ya CCM kujeruhiwa vibaya kwenye uchaguzi 2010.

  Tutakumbuka kuwa agenda hii ilitumika sana kuwa CHADEMA ni chama cha Wakristo na hata tumeona kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga mambo yalivyofanyika baada ya CCM kufanikiwa kukipaka matope CUF kwamba ni chama cha Kiislamu. Kwa sera yao ya udini, sasa wameamua kuhamishia majeshi yao CHADEMA baada ya kufanikiwa kuisarambatisha CUF.

  Udini unatumiwa na CCM kama kielelezo kwamba serikali inasemwa na kusimangwa sana kuhusu ufisadi kisa Rais ni Mwislamu, hata sasa hivi kuna watu wanazusha eti Mkulo (Mustafa) alihujumiwa kisa ni Mwislamu.

  Kwa kuwa CCM wameshindwa kutimiza ahadi zao kama Maisha Bora kwa kila Mtanzania, wameamua kutumia udini kama sera ya kulinda uzembe,ufisadi na maovu yao! Kiongozi Mwislamu akishindwa kutekeleza wajibu wake akishughulikiwa wanasema ni kwa sababu ni Mwislamu.

  Agenda ya Muungano imeingizwa kwenye suala hili la udini, kuwa umetawaliwa na mfumo wa Kikristo, na Tanzania Bara imejaa Wakristo, na wanaichafua Zanzibar, kwa hiyo ukiua Muungano Ukristo utakosa nguvu Zanzibar.

  Haya ni matunda ya kukua kwa mbegu ya udini iliyopandwa na watawala wetu mwaka 2010. Niliandika katika gazeti hili katika safu hii Januari 29, mwaka huu, niliona mbali na kutabiri hili kutokea Zanzibar kwa sababu nilishaona jinsi CCM na viongozi wake wakuu walivyoutumia mtaji wa udini.

  Serikali inafikiri kuwa kuwagawa Wakristo na Waislamu, ikapandikiza chuki itafanikiwa kuwatawala daima! Amani ni muhimu!

  Nchi za Afrika ya Magharibi zina Waislamu tena wenye imani kali kuliko Tanzania, Afrika ya Kaskazini na hata Bara la Asia kumekuwa na machafuko na vuguvugu la kudai mabadiliko kwa muda mrefu, lakini hata siku moja hawajawahi kuchomeana makanisa au nyumba za ibada.

  Wananchi wa huko hawakubali kugawanywa kwa itikadi za kidini kama hapa kwetu, wanaungana, wanajenga hoja wanaamua kudai mabadiliko na kuuwajibisha uongozi.

  Kila Mtanzania anajiuliza Zanzibar hawataki Muungano au hawataki Makanisa? Je, tatizo la Muungano ni Ukristo? Je, Ukristo ukiondoka tatizo la Muungano litamalizika?

  Viongozi wetu wanachochea, wanachekelea na wanafikiri wameshinda.Watanzania waachwe wajadili,waelimishane, wakemeane kama Watanzania bila kujaili dini na kama hawautaki Muungano waseme waziwazi.

  My concern

  CCM ni wadini wakuu katika nchi hii
   
 2. N

  Nsaji Mpoki JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2012
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 396
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ni vema kutofautisha vitendo vya kihuni na vile vya kiimani. Kinachotokea zanzibar hakina uhusiano kabisa na imani na wala hatuna haja ya kuupa picha mgogoro huo kuwa ni wa kidini. Kuna taarifa kuwa kule wilaya ya mufindi katika kijiji cha Rungemba mkoani Iringa Kanisa la Anglican limechomwa moto. Je huu nao ni mgogoro wa kidini?
   
 3. okaoni

  okaoni JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2012
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 1,197
  Likes Received: 466
  Trophy Points: 180
  What is happening in zanzibar is the effect of 10th zanzibar constitutional ammendment
   
 4. GEMBESON

  GEMBESON JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2012
  Joined: Apr 15, 2012
  Messages: 256
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Naona Kama kuna kaukweli vile!
   
 5. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Ndo matunda tunayovuna kutoka kwa uongozi wa jk
   
 6. b

  baraka moze Member

  #6
  Jun 3, 2012
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  hawajui kutenganisha siasa na udini
   
 7. a

  adolay JF-Expert Member

  #7
  Jun 3, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,595
  Likes Received: 3,074
  Trophy Points: 280
  CCm wanatumia silaha ya udini kuhalalisha na kuendeleza utawala wao lakini kwa msaada wa viongozi wa dini

  1. Mmoja wa viongozi hao ni MZEE WA UPAKO anatumika sana kushambulia wengine wanapoikemea na kuikosoa serikali ya CCM. (Anatumika tena vibaya na mungu hapendi kabisa)

  2. Baadhi ya mashehe sehemu mbalimbali za tanzania yetu, mfano mmojawapo ni kule Arusha wakisema tu wengine utasikia wanasema hii insemwa kwasababu Rais ni mwislamu.

  Taifa linateketea viongozi dhaifu na wabinafsi wanatetea upuuzi bila kupima madhara ya huu mfumo CCM na madhara ya sera ya divide and rule them kwa udini kwa amani na mstakabali wa vizazi vyetu hapo baadae.

  Ilikuwa CUF enzi za omari mahita mpaka majambia feki yakatolewa CCM ikashinda

  Imekumbwa CHADEMA tumeona rais mwenyewe akiruka kila kona kuna hila za kidini, kunahila za kidin, Kikwete huyu huyu baadaye akashinda kwa msaada wa viongozi wa din wachumia tumbo.

  Sasa maji yamezidi unga, kipimo kilele umpimiacho adui yako ndicho mungu atakupimia, Zanzibar haikamatiki na raia wamechanganyikiwa wanatekeleza sera ya udini, kisingizio muungano how????? burning churches has nothing to do with muungano.

  Huwezi hoji kwa kuungua kanisa moja kijiji cha Rungemba mkoani Iringa Kanisa la Anglican na makanisa zaidi ya ishirini huko zanzibar, kimahesabu lazima uwe wrong. ratio ya 1:26 ??? the probability of higher occurency will justfy the fact and signify the real root cause and not micro minority.

  Ni rahisi sana kutengeneza matatizo lakini kupata solution yake ni kazi kubwa. CCM imeasisi udini watu wanaimplement sasa je inaweza kureverse?? ni gharama kubwa.
   
 8. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #8
  Jun 3, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Ni kweli.Bahati mbaya sana watanzania wameanza kuingia kichwakichwa kwenye hako kamtego.
   
 9. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #9
  Jun 3, 2012
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 702
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hivi kweli mkuu tatizo haswa hulijuwi au unataka kutupumbaza ? Makanisa yapo Zanzibar kabla ya muungano hauna nia ya kuwepo.Wazanzibari kwa miaka nenda miaka rudi wanaishi na wakristo, wanasoma nao maskulini na jaribu kuwauliza labda ukipata nafasi kama waliwahi kubaguliwa na wanafunzi wenzao.

  Personally, nimesoma na mkristo kwa miaka minne.Na nilikuwa nashirikiana kama mwanafunzi mwengine yoyote yule.

  Tusijaribu kukimbia hoja ya msingi, yaani "mamlaka ya watu wa Zanzibar kujiamulia masuala muhimu ndani ya nchi yao"..Hususan suala la uchumi na sera zake, siasa na upatikanaji wa viongozi...pitia hio orodha na ongezeko la mambo ya muungano kupata hisia kamili.

  Wengi wameshachoshwa na mfumo uliopo, aidha njia inayotumika kudai ni sahihi ? Labda tujiulize kama njia hii unaona sio sahihi, nyengine iko wapi ?

  Mie nakubaliana na njia iliopo itumike hio hio, hata kama itakuwa ni kwa jukwaa la dini.Kwani nani alisema ni uhaini kujadili muungano ? Kama walio wengi wanataka muungano, basi wacha tuende kwenye referendum, halafu hao wengi wataonesha makali yao.Kama JK anahisi kujadili muungano ni sawa na kukufuru, basi tuendelee tuu.Wala msidhani kama uvunjikaji wa amani Zanzibar, basi Tanganyika itakuwa salama.

  Vyovyote iwavyo, hata Tanganyika inategemea utalii.Jaribuni kufanya utafiti,utagundua watalii wote wanaopanga safari za mbuga...basi wakitoka hapo huelekea Zanzibar.Huo ni mfano tuu, lakini yapo mengi.Msije sahau tuu kuwa Zanzibar ikichafuka, na Tanzania pia imechafuka ? Mfano kamili ni wakimbizi wa machafuko ya uchaguzi, hawa hawakuwa wakimbizi wa Zanzibar...bali wa Tanzania.

  Wasalaam,
   
 10. Macos

  Macos JF-Expert Member

  #10
  Jun 3, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 1,831
  Likes Received: 1,004
  Trophy Points: 280
  Uamsho ulikua na kibali kamili cha kufanya mkutano huko lumumba na washiriki walifanya maandamano ya amani kuelekea kwenye mkutano wao .maandamano hayo yalibandikwa jina la matembezi ya amani yalikwisha salama na waandamanaji wakarudi majumbani, lakini baada ya muda, kulizuka ghasia muda mfupi baada ya kiongozi na mhadhiri wa Jumuiya ya Uamsho, Sheikh Mussa Juma kukamatwa kwa kwa udhalili kabisa, alikua ndani msikiti wakaja askari na wakamchota kama jambazi au mwizi na kutupwa ndani ya gari la polisi na kupigwa mabuti ....alikua msikitini akisomesha wakati huo...huu ni uhuni wa polisi , ushenzi dhidi ya kiongozi maaruf anae heshimika sana na wazanzibari..
  haya ndio yaliwakera waislam wa zanzibar, uhuni huu ndio ulioleta fujo na ghasia hizi...police kama kawaida wakimkamata kiongozi wa kikristo kwa ajili ya mahojiano huitwa kwa nidhamu lakini sio kwa viongozi wa kiislamu..hili lilileta hasira ya waislam wa zanzibar ..ni uhuni wa police ..ukweli ndio huo...walichochea hasira..ya raia
  Kiongozi huyo alipelekwa katika Kituo cha Polisi Madema Mjini Zanzibar na kusababisha mamia ya vijana kufika katika kituo hicho wakitaka aachiwe, na waliapa kutoondoka kituoni hapo hadi asubuhi, kitendo ambacho kiliwalazimisha polisi kurusha mabomu ya machozi usiku kucha na vurugu hizo kuendelea hadi siku ya pili. na katika hili watu wengine wakachoma makanisa ili kupaka matope harakati za Uamsho kuhamasisha raia kudai zanzibar yao.
  mengine hayo hayo ulio andika ni kujifurahisha tu
   
Loading...