Vurugu ya shopping ya sikukuu......... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vurugu ya shopping ya sikukuu.........

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by The Boss, Sep 8, 2010.

 1. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Kuna mambo mimi huwa hata siyaelewi kwa kweli......
  Sometimes mimi huwa najiona tofauti sana na watu wengine....


  Sasa hivi utakuta watu wengi wako bize kwa
  shopping....ukiwauliza watakwambia

  sababu ya sikukuu......

  Wengine wanasema ni kwa ajili ya watoto.
  Wengine utasikia eti' mke wangu hatanielewa nisipompa pesa
  ya shopping ya sikukuu'

  sasa ukienda kariakoo now au mlimani city na kwengineko......
  Utakuta watu wamefurika....
  Kariakoo sasa hata pa kupita hakuna........

  Ukiuliza kuna nini....
  Unajibiwa si sikukuu imekaribia........
  Na kipindi cha xmass ni hivyo hivyo.....

  Sasa mimi najiuliza ni lazima watu wafanye shopping
  kila sikuku zinapokaribia???????

  Kwa nini mtu usifanye shopping zako mapema
  na kwa ratiba zako??????

  Watu kujazana madukani,kwanza
  bei za vitu zinapanda karibu mara tatu,hasa nguo za watoto...

  Halafu hatari ya kuibiwa pesa kipindi hiki ni kubwa sana na utapeli mwingine.....

  Mwisho kwani lazima kila ikifika sikukuu ndio
  ufanye shopping????????????

  Kuna wanawake wengine ni kama watoto.......
  Na wao wanataka shopping ya sikukuu........

  Binafsi huwa nachukia sana kuona watu wanajazana mitaani

  eti ukiwauliza utasikia......sikukuu imekaribia....
  Yaani pilikapilika na foleni zisizo na lazima kabisa......
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Wakati wa sikukuu familia zinapata fursa ya kukaa pamoja na kufanya lolote la kufurahishana!

  Kutokana na mfumo wa maisha kuwa na shinikizo nyingi za kuzikabili,unakuta watu wanakuwa bize, wengine huenda mbali na nyumbani ili kupata riziki!...

  Lakini wakati wa sikukuu hujitahidi kuwapo nyumbani pamoja na familia zao ili kutathmini pamoja maendeleo yao, na si mbaya kama watafanya shopping na kupendeza kwa pamoja!-Thats My take!
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Ishu hapa si kukaa pamoja...
  Ishi kukuta watu wamejazana kariakoo na kwingineko
  mpaka hakuna pa kupita kwa sababu ya shopping tu ya sikukuu....
  Kusherehekea pamoja unaweza kusafiri na familia yako au kualika
  watu nymbani kwako mkasherehekea.......

  Mimi nachopinga hapa kusababisha misongamano isiyo na lazima......
   
 4. doup

  doup JF-Expert Member

  #4
  Sep 8, 2010
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  urith wetu, sijui kama nchi za wenzetu huu ni utamaduni pia, tulishaazoenshwa kila sikukuu nguo mpya, ukibahatika siku za kawaida ni mtumba
   
 5. k

  kisukari JF-Expert Member

  #5
  Sep 8, 2010
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,761
  Likes Received: 1,051
  Trophy Points: 280
  ni kweli kwani kama uwezo wa maisha ni mdogo,siku ya sikukuu ni siku ya kupata kama nguo mpya au kula pilau,hasa kwa watoto wadogo siku hiyo wanajihisi special.na kufanya shopping kipindi hicho,kwa sababu pesa kama unaenda kukopa,utakopa sababu ya sikukuu kwa hiyo inakuwa ni kipindi hicho,na kama unazichanga pesa,zinakamilika kipindi hicho cha karibu ya sikukuu. Lakini kwa watu wenye uwezo wao,siku yoyote zinanunuliwa nguo mpya au kula vizuri ni kila siku sio siku ya sikukuu tu.
   
Loading...