Vurugu na Mapigano baina ya wafuasi wa CCM na CHADEMA Kyerwa Karagwe

Mathias Byabato

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
1,020
691
Jana usiku kulitokea mapigano na vurugu kubwa katika jimbo la Kyerwa mkoani Kagera baada ya misafara ya wafuasi na wapambe wa wagombea udiwani kata ya Bugomora kugongana na kuanza kushambuliana, vurugu zilikuwa kubwa, nyumba kadhaa zimechomwa moto na baadhi ya magari kuharibiwa.

Polisi kutoka kituo cha Mulongo walifika katika eneo la tukio usiku na kutuliza ghasia lakini mali kadhaa zilishaharibiwa, hakuna kifo wala majeruhi.
moja%2Bmoja.jpg

Mali ya mgombea wa CHADEMA YALIYOHARIBIWA

Habari ambazo mtandao huu umezipata muda huu zinasema kuwa katika kijiji cha Nyamiyaga Kata ya Bugomora wilayani Kyerwa watu wanaosadikiwa ni wafuasi wa CCM NA CHADEMA wapo wanapigana vurugu zilizoanza saa majira ya saa kumi na mbili jioni hii ambapo magari 3 yamevunjwa vioo na nyumba kadhaa zimeishabomolewa.Shuhuda wetu anasema amewasiliana na
mbili%2Bmbili.jpg

Magari yaliyoharibiwa mali ya Mgombea wa CHADEMA Kata Bugomora ambaye ni diwani anayemaliza muda wake

Jeshi la polisi wanatoka kituo cha Mpakani mwa Tanzania na Uganda habari zaidi tukizipata tutakujuza kinachoendelea

Update za hivi punde ni kuwa misafara ya wagombea imekutana kwenye senta ya Nyamiyaga sokoni mgombea wa CCM Zzawadi Niclous Kazahura alikuwa na mkutano kijiji cha Nyamiaga alipo maliza mkutano aliondoka wakawa wanacheza muziki wao hapo senta na mgombea udiwani CHADEMA Tulakile Twijuke Libent alikuwa na mkutano kijiji cha Magoma nao walipitia senta hapo maana mgombea huo makazi yake yapo hapo ndipo zilianza kupigwa magari manne yameharibiwa sasa ni kurushiana mawe.

Askari bado hawajaripoti kwenye eneo la tukio. Polisi wamefika eneo LA tukio muda huu na wanajaribu kutuliza ghasia ila pikipiki mbili za diwani wa Chadema zimechomwa pamoja na duka lake hali ni tete tutakujuza na picha utazipata baadae

updates:
Polisi wamefika eneo la tukio na kutuliza ghasia lakini duka na pikipiki kadhaa mali ya mgombea diwani wa kata hiyo kupitia CHADEMA tayari vimekwisa teketezwa kwa moto .

Jeshi la Polisi toka makao makuu ya wilaya ya Kyerwa na Makao makuu Mkoa wa Kagera wapo eneo la tukio wanaendelea na kuwatafuta waliohusika na tukio.


Tutaendelea kukujuza linalojri.


Chanzo: somahabari
 
Kyerwa hilo ni jimbo la Ukawa watawakamua Magamba vizuri ndio mana wahaha sana
 
Kwa sasa hali ni shwari kulingana na taarifa tulizopata kutoka kwa waandishi wa redio fadeco walioko eneo la tukio
 
Ukisikia viongozi wakuu wanaema " huyu kahamia upande wa maadui nae ni adui yetu" ujue upinzania ni uadui na haya ndo mategemeo... viongozi tunzeni ndimi zenu... tz ni yetu wote na siasa sio u adui. ...
 
Mliopewa wadhifa Wa kutuongoza tumieni busara kwenye maamuzi yenu na hofu ya Mungu iwe juu yenu
 
Ilihali hakuna mwana ccm au mali ya ccm iliyoharibika,nawapongeza vijana wa ccm waliopo eneo hilo kwa kujibu vyema mashambulizi.
 
Back
Top Bottom