Vurugu kati ya CHADEMA na CUF juu ya USHOGA zasababisha Bunge kuahirishwa

HAKI SAWA KWA WOTE?
Kumbe CUF mna ajenda zenu binafsi, Lipumba alisema msikitini na kuwahadaa watanzania wenzetu waislamu kuwa wakiogope chama chenye mahusiano na vyama vya nchi za magharibi kumbe ulikuwa ni unafiki na ufitini maana HATA CUF WANA VYAMA MARAFIKI VYA NJE TENA VYENYE MALENGO HASI KAMA YA USHOGA.

Thanks Dr.Wenje.
 
So Chadema ni chama cha KIKRISTO nakunukuu tu.... na hakirusu ushoga!!! mkuu uchaguzi wa nini na wapi pa kusemea ndio ukomavu kisiasa la sivyo yataendelea kutokea kaa yaliyotokea.....

According to Wenje, CHADEMA kinafuata itikadi ya kikatoliki yaani political catholism chini ya mtendaji wake mkuu padri mstaafu aliyesomea na kubobea vyema hadi ngazi ya udocta ya cannon law.
 
Tatizo hapa ni uelewa mdogo wa wanasiasa wetu.Ukweli ni kwamba vyama vyote vya kiliberali vanatetea haki za binadamu hata zilizoopitiliza ikiwemo kuruhusu haki za ndoa za jinsia moja.Lililoelezwa ndani ya bunge ni ukweli usiopingika ila pengine neneo ushoga na usagaji hawalitaki litamkwe hadharani.Pengine pia aliyeomba mwongozo haelewi chama chake kina ushirikiano na chama chenye mrengo upi.Lakini ninavyofahamu mimi vyama vya kiliberali huo ndio mrengo wao na hapo ndio natia shaka kama vyama vyetu hapa nchini vinachambua kwa undani miirengo ya vyama wanavyoshirikiana navyo au wanakurupuka kwa ajili ya kujipatia fedha na misaada.
 



chadema kuwa na ushirikiano na CDU inamaana Chadema ni chama cha kikristo ...! ?

Tatizo mnatumia jazba, unajua ukiisoma vizuri ile hotuba hamna mtu aliye sema CUF ni chama cha kishoga, ila marafiki zake ni waleberali na ni vyama vinavyounga mkono ushoga, kwahi sasa CUF ilitakiwa wajibu kisayansi kwamba wana marafiki wanaounga mkono ushoga ila wao hawaungi mkono ushoga na wakaelezea ni kivipi? vinginevyo CUF safari hii wameshikwa pabaya sana, mlikosea sana kumruhusu Lipumba kwenda kumwaga Pumba kwenye misikiti
 
hivi ile ndoa iliyofungwa kati ya cuf na ccm ni ya jinsia ngapi? mwenye uelewa anisaidie jamani.
 
Hili bunge ambalo kila yanapotokea majibizano makali linaahirishwa kabla ya muda muafaka, litawezaje kufikia malengo yake kwa muhula/term/mwaka?
Au ndio chama tawala kina take advantage ya kukimbia hoja muhimu zisijadiliwe?
Namna hii safari ni ndefu mno.
 
CDM ngoma ikivuma sana mwishowe inapasuka sasa nyie mnathubutu kuhoji swala hilo mmesahau uhusiano wenu na CDP cha ujerumani na swala la udini? pia mmesau ukaribu wenu na David Cammeron? hahaha kweli shukrani kwa wenje kuwafanya watanzania wafikiri zaidi haswa issue kama ile ya Nape then Dr akampa siku 14 hadi sasa hazijafika na hakuna majibu ya kuridhisha juu ya ukaribu wenu na CDP.

Makene vip umeenda kumuuliza Dr nini cha kuandika.Mmelikoroga
 
Tumaini....

Hoja ni Wenje kuwatuhumu CUF kushirikiana na Waliberali ambao anadai wanaunga mkono ndoa za mashoga na wasagaji ilhali chama chake (CHADEMA) nacho kina uhusuano na chama cha 'Wahafidhina' - Conservatives ambao pia wanaunga mkono ndoa za jinsia moja na ilifikia kipindi PM wa Uingereza David Cameron ambaye ni kiongozi wa Conservatives alitishia kutotoa misaada kwa nchi ambazo hazitaunga mkono/kupinga ndoa za jinsia moja....

Sidhani kama kuwa na ushirikiano na chama kinachounga mkono ushoga nawe utakuwa unaunga mkono ushoga...Ni sawa na CHADEMA kuwa na uhusiano na chama cha kikristo cha CDU cha Germany halafu mtu aseme CHADEMA waafuata itikadi ya udini....Hii haitakuwa sahihi....

Wenje na kambi yake wangeweza tu kutumia busara na kutoliweka hili kwenye hotuba yao....Maneno yaliyopo kwenye hotuba hiyo ni makali mno na yanachoma......

Bala.

Dawa ya luba ni mruturutu, CUF wamelikologa wanapewa walinywe wana toa mapovu. Walikwisha ambiwa mapema na Bi Kiroboto...'mkuki kwa nguruwe..'

Mweshimiwa Balantanda, weka links kawa wenzako kuthibitisha unachokiamini na sisi tufuatilie, vingivenyo utakuwa ni mpiga ramli!
 
What Liberals says about Mariage:
Marriage is the union of people who love each other. It should be legal for gay, lesbian, bisexual and transgender individuals, to ensure equal rights for all. Support same-sex marriage. Opposed to the creation of a constitutional amendment establishing marriage as the union of one man and one woman. All individuals, regardless of their sexual orientation, have the right to marry. Prohibiting same-sex citizens from marrying denies them their civil rights

Then what CUF says about haki:
Haki sawa kwa wote, ikimaanisha haki sawa kwa mashoga, wasagaji, walemavu, walevi, weupe, weusi etc etc

FACT:
BASING ON THIS FACT HAKUKUWA NA HAJA KWA MBUNGE NA WABUNGE WA CUF KUANZA KUTUKANA NA KUITUKANA CHADEMA NA WENJE.
 
Tuache ushabiki. Wapi pameandikwa cuf ni chama cha mashoga hapo? Pameandikwa cuf ni chama cha kiliberali . Halafu msingi wa uliberali na vyama vingne vya kiliberali duniani. Mbna jusa,lipumba n.k wanakipambanua chama chao kua ni cha kiliberali. Je akisema 'wenje' cuf ni waliberali ndio inageuka kua lugha ya kuudhi?. Liberal msing wao mkubwa ni 'liberty'. Maana yake ni 'liv as u wish'..hawa wanataka mwanadamu awe huru kuamua chochote anachojisikia. Katika swala la mahusiano,wanataka mwanadamu awe huru kuchagua, kuoa jinsia yake au vinginevyo.! Sasa cuf ni liberal paty! Kuna dhambi kuwaita liberal!
hivi wewe umeelewa zaidi ya wana cuf wote kule mjengoni?
 
Subiri waje hao CCM-B. Misaada ni kitu kibaya sana , yaani CUF wanaunga mkono ushoga sababu ya pesa.
 
Mbona unakuwa mgumu kuelewa ndugu? Kwa faida ya watanzania wote Mhe. Wenje aliamua kuelezea itikadi kubwa tatu zilizopo hapa duniani. Hivyo ni jukumu vyama vyote vya siasa hapa Tanzania kupambanua kwa uwazi juu ya sera zao,
badala ya kufanya propaganda ambazo hazina tija kwa wananchi kwa mwisho wa siku wananchi watafanya maamuzi nani anafaa kuwaongoza,

Sasa ni nani mgumu wa kuelewa kati yetu? Wenje amesema CHADEMA ianpinga ushoga na usagaji akiwa anamaanisha wale wanaofuata liberalism wote wankubali ushoga na usagaji.

CHADEMA inajiongezea idadi ya maadui badala ya marafiki!

Lakini kwa kujificha itikadi yake Wenje hakuthubutu kutaja CDU kama miongoni mwa washirika wake akidhani watu hawajui!

CDU katika Part Platform yake kinajibainisha kama chama cha fiscal and national conservatism itikadi ambayo iafuatwa na CHADEMA. Lakini pia sera za CDU zinatokea kwenye ukatoliki.

Vipi hapa CHADEMA inataka kuwaambiaje watanzania kwamba chenyewe ni chama chenye malengo ya ukatoliki?

Bear in mind kwamba katibu mkuu DR W Slaa, ni alumni wa baraza la maaskofu (TEC)!
 
Mkuu Makene,
Ni wazi hii hotuba ilikuwa na lengo la kuwahusisha CUF na Ushoga. Hizi ni cheap politics ambazo haziisaidii kabisa nchi yetu.

Kwani wanaounga Ushoga huku Ulaya ni Liberal tu? Mbona Conservative wa UK ambao pia wana uhusiano na CHADEMA ndio wamepeleka sheria bungeni ya kuruhusu ndoa za Ushoga? Tena juhudi hiyo inaongozwa na kiongozi wao wa chama ambaye pia ni waziri Mkuu wa nchi.

Kama katika uhusiano wowote haina maana unakubaliana na kila jambo analofanya rafiki. Muhimu ni kuambiana ukweli na kushauriana na pale inapotokea kushindwa kuwa na msimamo mmoja basi kukubali kutofautiana.
Wenje amejibu hoja tena kwa kutumia facts na sio myths.
Ni CCM na CUF vimekuwa vikieneza propaganda chafu ndani ya Bunge na mitaani kuwa CHADEMA kinapaswa kufutwa kwa kuwa ni chama kinachopewa misaada kutoka nje tena kwenye vyama vya mrengo wa kidini na Mashoga hivyo wataleta udini na ushoja nchini!!!
Sasa leo Wenje kaamua kujibu hoja kwa uwazi.

Wenje kazungumzia Itikadi ya Kiliberali imbayo inatetea ushoga, lakini pia CUF ni chama chenye itikadi ya Kiliberali na juzi tu imepokea msaada kutoka vyama rafiki vya kiliberali vya huko Ulaya.

Kosa likwapi au Uongo uko wapi hapo?
 
According to Wenje, CHADEMA kinafuata itikadi ya kikatoliki yaani political catholism chini ya mtendaji wake mkuu padri mstaafu aliyesomea na kubobea vyema hadi ngazi ya udocta ya cannon law.
Usipotoshe jamii inayokuzunguka.Ccm wako madarakani kwa muda mrefu na umesahau kuwa Waziri Membe alipingana sana na Waziri Cameroun wa Uingereza kuhusu kupewa misaada mpaka turuhusu ndoa za jinsia moja.Hivyo Tanzania ni nchi isisyoruhusu ushoga na usagaji ikiongozwa na ccm.Je ccm nayo na chama cha kikatoliki kwa sababu kinapinga ushoga?Je Uislamu unaruhusu ushoga?MBONA MNATUPOTOSHA?
 
sijaona kabisa mahari ambapo wenje amewatuhumu CUF kuwa ni chama cha mashoga nilichoona ni kwamba ameetueleza tu mlengo wa chama cha CUF,CCM na CDM sijaona ubaya kabisa
 
Back
Top Bottom