Kyindokyakombe
Member
- May 1, 2012
- 95
- 96
Wafugaji wanapendelewa na mkuu wa wilaya na mapolisi kwa kuwa wanahonga sana.
Mgogoro wa eneo hilo na wilaya ya Kilosa kwa ujumla ni mkubwa sana na wa miaka mingi sana (Nilishawahi kufanya research huko 2003 kuhusu migogoro ya ardhi). Inashindikana kutatuliwa kwa kuwa wafugaji wana uwezo wa kuhonga wakati wakulima hawana uwezo wa kuhonga.
Kumbukeni mgogoro wa Msovero mwaka 2001 ambako watu zaidi ya 100 walikufa. Serikali ya CCM imekuwa ikumbatia hii migogoro bila kutafuta suluhisho la kudumu. Pia mapendekezo ya sheria ya ardhi ambayo yangemaliza kabisa migogoro hii ya wakulima na wafugaji yalikataliwa na wabunge wanaotokea maeneo ya wafugaji kwa kuwa ingewanyima haki ya kugeuza nchi nzima eneo la malisho.
Serikali ya CCM imeshindwa kuleta maendeleo na inashindwa hata kutatua migogoro ya ardhi. Shime watanzania tuikatae CCM
Picha pia hujaeleweka kabisa
Msijali,huo ni upepo tu unapita, nchi yetu ni kisiwa cha amani na utulivu, ambapo hadi nchi jirani zinazotuzunguuka wanatuonea wivu!!!Kuna maandamano yamefanywa na wananchi eneo la Dumila.
Chanzo ni mgogoro kati ya WAKULIMA na WAFUGAJI. Makazi ya wafugaji yamechomwa moto.
Mpambano unaendelea wananchi wamebeba silaha za jadi wanaelekea kituo cha POLISI.
Hizi ndizo athari za kula 'mlungula' kwa watawala wenye uwezo wa kutawala familia. Rejea kauli ya Mh. Kafulila aliyowahi kuitoa bungeni juu ya madhaifu ya watawala.
Wewe mbona unachoongea kipo nje ya topic? Au bado una hang'over ya mataputapu, uliyoyatandika jana usiku??!!
wilaya ya kilosa ni wilaya inayoongoza kwa ufisadi ndo maana haya yote yanatokea, sasa mtu mmja anasababsha uharibifu mkubwa wat wamejaza miti,mawe,machuma barabarani