Vunjeni Muungano lkn mimi nitabaki Mtanzania


Ahsante sana Taso kwa uchambuzi wako.

Hakuna ubishi kwamba Muungano ni ndoa ya kulazimisha. Ni kiloba cha misumali. Labda tujiulize kitu kingine...Nani analazimisha kuendelea kuwemo katika hii ndoa batili na kwa maslahi gani?
 
Ahsante sana Taso kwa uchambuzi wako.

Hakuna ubishi kwamba Muungano ni ndoa ya kulazimisha. Ni kiloba cha misumali. Labda tujiulize kitu kingine...Nani analazimisha kuendelea kuwemo katika hii ndoa batili na kwa maslahi gani?

Wakuu wa CCM/SMZ/SMT ambao wanafaidi sana.
 
Wakuu wa CCM/SMZ/SMT ambao wanafaidi sana.

Sasa mbona hata hao wakuu wa SMZ wanalalama? Huu muungano umekuwa kama toto lisilo na busara ambalo halijui jinsi wazazi wanavyohaingaika usiku na mchana ili liwe na maisha mazuri. Lenyewe linaishia kulalama kila saa kwamba wazazi hawafanyi hili au lile. Dawa yake ni kuliachisha kunyonya ili liingie lenyewe mtaani likajaribu upande wa pili wa maisha.

Ningefurahi sana kama muungano huu tulionao ungeisha leo. Huu ni dizaini ya mtoto si riziki...Ufe ili tuanze upya kila mtu kivyake vyake au turudi kwenye drawing board!
 
Vunjeni huo muungano wa kinafiki, hatuutaki tumechoka kunyonywa na wazanzibari. Haiwezekani zanzibar yenye idadi ya watu milioni moja wanawabunge 50, wakati Tanganyika ina watu milioni 43 ina wabunge 289. uwiano hakuna ondokeni nyie wazanzibari, kama ni kulinda mpaka tunao makorokoroni kibao tena wana nguvu.
 

Maneno kama haya tena yakiwa yanatoka pande zote za Muungani ni dalili tosha kwamba watu wamechoka na wako tayari kuitapika nyongo. Laiti wakubwa wangeyajua haya, tena bila unafiki na maslahi binafsi...Tungemalizana na hizi karaha leo!
 
Ahsante sana Taso kwa uchambuzi wako.

Hakuna ubishi kwamba Muungano ni ndoa ya kulazimisha. Ni kiloba cha misumali. Labda tujiulize kitu kingine...Nani analazimisha kuendelea kuwemo katika hii ndoa batili na kwa maslahi gani?

siku zote kuungana ni jamboi muhimu ndugu na nchi zote zilizoendelea zimeungana
kuna USA, UNITED KINGDOM, EUROPEAN UNION, KULIKUWA USSR. LKN TATIZO TULILOKUWA NALO SISI NI MFUMO WA MUUNGANO WETU. inavyotakiwa ni kuungalia upya muungano na kungalia mapungufu yake na vipi tutauboresha.
 
Bora muungano uvunjike unguja irudi kwa waarabu, huu muungano umeirudisha nyuma zenj.
 

kaka sikatai kama hayo uliyoyasema si kweli inawezekana kweli lkn mtoto akinyea mavi hatukati mkono huwa tunauosha mkono. so tunachopaswa kufanya ni kuangalia ni mapungufu yapi ukimuiisha hayao uyasemayo wewe kwa maoni tukaangalia ni jinsi tutayarekebisha ili kila mmoja akanufaika na huu muungano wetu. narudia tena kuungana ni jamboa jema ila the way tulivyoungana ndio tatizo so turekebishe hizo kero zetu.
 
Hivii, naweza kuruhusiwa kugombea uwakilishi au ubunge huko Zenji bila kikwazo?

hahaha.. mkuu sahau hilo... kamwe huwezi.. Lakini mzanzibar anaweza kugombea bara na akakubalika... angalia hussein mwinyi tuvunje muungano kila mtu achukue chake.. tubakli nchi jirani
 

Hilo pendekezo lako ya kuungalia muungano tayari limepitwa na wakati. Tayari watu wameshachoka. Utawezaje kufanya hivyo? Labda ingewezekana kwanza kupeana talaka rejea.

Kama viongozi wa juu kabisa wa SMZ wanaweza kusema maneno makali kama wanayoyasema sasa; Hapo hujaongelea wananchi wa kawaida, sina hakika kama huu muungano unaweza kuokolewa kwa sasa. Tuukubali ukweli ili tuanze upya ..bara kivyake vyake na Zanzibar kivyao ili ikibidi tuungane tukiwa sober. Kwa sasa sidhani kama kuna mtu yuko tayari kusikiliza hizo hadithi za kuungalia muungano kwani nafasi adimu zilizokuwepo huko nyuma zilichezewa. I think it is too late!
 

Practially siyo rahis tena kumaliza kero za muungano bila kuuvunja kwanza au kurudi kwenye drawing table kuamua kama tunautaka na kama kweli pande zote zinautaka basi tutakakubaliana muundo mpya.

Huu wa sasa hauwezi kuwa-rehabilitated. Ni kama tunavyoongelea katiba yetu.. We need to start upya kabisa. La sivyo tunazidisha ukubwa wa jipu..na kuzidi kuomba Mungu lisipasukie mbele yetu...Too bad kuwawekea wajukuu zetu matatizo yasiyo ya lazima!
 

Nimesha changia thrd hii lakini sasa naona kama nilipoteza muda maana naona kama imeandikwa na mtoto!

Huyu 'mtoto' hakuwa na hoja yoyote ya kujadili. Anaeleza udhaifu wake na mfadhaiko, nk. Naona tumeendelea kuchangia kwa kukumbuka umuhimu wa jambo la Muunganao na mjadala wa katiba unaoendelea sasa hivi. Tumuache aendelee kuhangaika na mambo yake maana hata hakusema sababu ya kutaka u-Tanzania wake kwa nguvu zote hizo.
 

ndugu kama wingi wa watu ndio kupewa priority basi INDIA walitakiwa wapewe kura ya VETO kwenye UMOJA WA MATAIFA. UNITED KINGDOM nayo haikutakiwa ipewe kura ya VETO kwani ina watu hawafiki milioni 70 wangepewa INDIA AMBAYO INA WATU KARIBU I BILIONI KAMA SIO ZAIDI.
 

na jingine tulivyoungana na zanzibar tuliungana na zanzibar kama nchi na sio mkoa. Kwahiyo mimi nahisi ili kuzuia huu mkanganyiko tunapaswa kuwa na mabunge matatu la tanganyika, zanazibar na bunge la muungano(tanzania) na raia wote watabaki ni watanzania.
 
Zanzibar inafaa iwe mkoa wa Tanzania ili kuwe na Muungano wa Kweli


Mkuu hilo sahau kabisa kabisa:

Katiba ya Zanzibar ya 1984 inasema;

(9)(i) Zanzibar itakuwa ni NCHI ya kidemokrasia na haki za kijamii.

(9)(2)(a) Mamlaka ya kuendesha NCHI ni ya wananchi wenyewe …

(10) Kwa madhumuni ya kuendeleza umoja na maendeleo ya watu na ustawi wa jamii katika NCHI itakuwa ni wajibu wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar:

(10)(3) Itadhibiti uchumi wa NCHI kufuatana na misingi na madhumuni yaliyoelezwa na katiba hii.

(12)(3) Haki za raia, wajibu na maslahi ya kila mtu yatalindwa na kuamuliwa na mahkama pamoja na vyombo vya NCHI na vinginevyo vilivyowekwa na sheria.

(21)(i) Kila Mzanzibari anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa NCHI…

(23)(2) Kila mtu ana wajibu wa kulinda maliasili ya Zanzibar, mali ya NCHI pamoja na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi…
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…