VPL, Yanga yabanwa mbavu kwa kulazimishwa sare 2-2 na Ruvu Shooting Uwanja wa Uhuru

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Mategemeo ya Klabu ya Yanga SC kumaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa Vodacom Premier League (VPL) yamezidi kufifia baada ya hii leo kulazimishwa sare ya 2-2 dhidi ya Ruvu Shooting.

Katika mchenzo huo ulikuwa wa ushindani timu zote zilianza kwa mashambulizi makali kwa pande zote. Lakini Yanga ndo waliokuwa wa kwanza kuandika bao dakika ya 19' kwa shuti la Matheo Antony.

Ruvu Shooting walisawazisha bao kunako dakika ya 30' kupitia kwa Mcha Hamis kwa mkwaju wa penati baada ya beki Abdallah Shaibu kuunawa mpira eneo la 18.

Yanga waliendelea kulisakama lango la Ruvu na walifanikiwa kupata bao la pili dakika ya 40' kupitia kwa Maka Edward.

Hadi mapumziko matokeo ubaoni Yanga 2-1 Ruvu Shooting, kipindi cha pili Ruvu walicheza kandanda la kushambulia hali iliyosababisha kusawazisha bao kupitia kwa Issa Kanduru.

Hadi kumalizika kwa mchezo huo Yanga 2-2 Ruvu Shooting, kwa matokeo hayo mechi ya Jumatatu ndo itatoa taswira timu gani itashika nafasi ya pili Kati ya Yanga SC na Azam FC baada ya Simba SC kunyakua ubingwa wa huo wa VPL.
 
Yanga Vs Ruvu Shooting
IMG_20180525_211352_034.jpg
 
Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema walikuwa na asilimia mia ya kuifunga Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, lakini waliwaonea huruma kwa kuwa wako katika matatizo.
“Pale Jangwani kuna shida, kuna matatizo na mambo si mazuri. Tulipaswa kuwa na huruma.


“Tulifuata maandiko ya Mungu, anasisitiza huruma. Kama si hivyo, tungewapapaa Yanga kama ambavyo tulikuwa tumeahidi,” alisema.
 
Back
Top Bottom