VPL: Tanzania Prisons (Wajela jela) waipigisha Gwaride KMC

Shadida Salum

Journalist at JamiiForums
Sep 11, 2020
69
104
20210212_185518.jpg


Baada ya kumnyuka Namungo bao 3-0 , leo KMC wamepoteza mbele ya Tanzania Prisons bao 2-1 mchezo uliopigwa katika dimba la Nelson Mandela huko Shmbawanga.

Jeremiah Juma alitosha kuiibua timu hiyo kidedea baada ya kuweka mpira wavuni mara mbili, kunako dakika ya 29 na dakika ya 50. Huku goli la kufutia machozi la KMC likifungwa na Israel Mwenda dakika ya 67.

Ikiwa ni mchezo wa kwanza kushinda kwa Tanzania Prisons tangu Novemba 29 , 2020, kwa matokeo hayo Tanzania Prisons inapanda kutoka nafasi ya 10 mpaka nafasi ya 7 kwenye msimamo wa ligi huku KMC wakiendelea kusalia katika nafasi ya 6.

Kwa upande mwingine Ihefu sc imemlazimisha Ruvu shooting bao 2-0 akiwa nyumbani katika uwanja wa Mabatini pwani.

Magoli ya Ihefu yamefungwa na Issa Ngoah dakika ya 21 na 90+2. Kwa matokeo hayo Ihefu inapanda kutoka nafasi ya 18 mpaka ya 16 ikiwa na alama 16 huku Ruvu shooting ikiendelea kusalia nafasi ya 5.
 
Back
Top Bottom