VPL: Simba VS Majimaji FC, Simba yairarua Majimaji bao 4-0 uwanja wa Taifa

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
a8e73919184e3b661cde54c80b6bbe4d.jpg
Patashika ya Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara (VPL), kuendelea leo kwa mechi mbili kupigwa katika viwanja tofauti. Katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Simba SC, watawakaribisha Majimaji FC, kutoka Songea, huku Tanzania Prisons wakiwa wageni wa Singida United katika uwanja wa Namfua mkoani Singida.

Je Tanzania Prisons wataweza kuwachezesha kwata walima Alizeti ama walima Alizeti Singida United wataibuka wababe?

Kocha Pierre Lechantre raia wa Ufaransa ataongoza rasmi kikosi cha Simba SC kwa mara ya kwanza je, wataeneleza ubabe wao ama watachezeshwa Lizombe na Majimaji FC?

Kumbuka kwamba shughuli yote ni kuanzia saa 10: 00 jioni. Kaa nasi kukuletea yatakayojiri. Usikose ukaambiwa.

Vikosi vya timu zote tukianza na wenyeji wa mchezo Simba SC;

Aishi Manula, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Juuko Murshid, Asante Kwasi, Jonas Mkude, Jamal Mwambeleko, Said Ndemla, John Bocco, Shiza Kichuya, Emmanuel Okwi.

Sub;

Emmanuel Mseja, Nicholas Gyan, Mohamed Hussein, James Kotei, Mwinyi Kazimoto, Mzamir Yassin, Laudit Mavugo.

Na kikosi cha Majimaji FC ambao ni wageni katika huo.

Salehe Malande, Lucas Kikoti, Mpoki Mwakinyuke, Kennedy Kipepe, Paul Mahona, Hassan Hamisi, Peter Mapunda, Yakubu Kibiga, Godfrey Mlawa, Marcel Bonventure, Japhar Mohamed.

Sub;

Andrew Ntala, Sadick Gawaza, Idrisa Mohamed, Six Mwasekaga, Jerryson Tegete, Alex Kondo.

======

Wakati wowote mpira utaanza hapa uwanja wa Taifa..

01' Mpira umeanza, Simba 0-0 Majimaji
04' Asante Kwasi anajaribu kuingia kwa kasi eneo la hatari la Majimaji lakini beki wa Majimaji anazuia
08' Emmanuel Okwi anapiga Mpira wa kichwa unaopaa juu baada ya kupokea pasi mzuri ya Shomari Kapombe.
16' Simbaa, Shiza Ramadhan Kichuya anapiga krosi nzuri na John Boko anaandika bao la kwanza baada ya gonga gonga nyingi langoni kwa Majimaji. Simba 1-0 Majimaji
23' Shomari Kapombe anaingiza krosi maridadi lakini John Bocco anapaisha juu ya goli.
26' John Bocco anaandika bao la pili kwa Simba baada ya kupiga kichwa krosi maridadi. Simba 2-0 Majimaji
31' Simba wanatawala mpira na kucheza pasi nyingi, wanapata kona ya Tano lakini haizai matunda.
45+3' Dakika 45 zinakatika, Simba 2-0 Majimaji.

======

49' Shomari Kapombe anapiga shuti Kali langoni kwa Majimaji lakini golikipa anafanikiwa kupangua.
53' Emmanuel Okwi anaandika bao la tatu baada ya walinzi wa Majimaji kutojipanga vizuri. Simba 3-0 Majimaji.
55' Simba wanatawala Mpira kwenye lango la Majimaji lakini umahiri wa Mlinda mlango unazuia bao jingine.
68' Okwi anaiandikia Simba bao la nne baada ya kazi nzuri ya John Bocco. Simba 4-0 Majimaji.


90+5' Mpira umekwisha, Simba anaibuka na ushindi wa bao nne bila majibu. Matokeo haya yanaipa Simba tofauti ya alama 5 kileleni.
 
Hapa pointi 3 ni lazima juu ya alama na kushika usukani bila bughudha..!

Asante Vyura kwa kurahisisha hilo kwa Azam FC
 
Moderates, ni uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, sahihisho kwenye heading
 
Mashabiki si wengi sana waliofika kushuhudia mtanange huu
 
5' Kona kuelekea upande wa Majimaji FC

Inapigwa konaaaaa la inaokolewa
 
Okwi anakwendaaaa la goal kick.. 10' Simba SC 0-0 Majimaji FC
 
Mwambeleko anakwenda la kona,

inapigwa konaaaaa la nje goal kick
 
14' Simba SC 0-0 Majimaji FC. timu zote zinashambuliana kwa zamu
 
17 'Go go Goooooooooaal John Bocco anaandika bao la kwanza kwa kichwa kufuatia kona iliyopigwa
 
Back
Top Bottom