Vodacom yamwaga vifaa Ligi Kuu Bara

Vodacom yamwaga vifaa Ligi Kuu Bara

Rugby Union

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2012
Posts
402
Reaction score
257
Vifaa_ligikuu.jpg

Vodacom ikikabidhi vifaa vya michezo kwa timu zitakazoshiriki ligi kuu ya Vodacom msimu ujao, Tanzania bara. ​

WADHAMINI wa Ligi Kuu Bara (VPL) Kampuni ya Vodacom, jana Jumatano ilitoa vifaa kwa timu 14 zitakazoshiriki ligi hiyo iliyopangwa kuanza Septemba 20, Vifaa hivyo vimegharimu Sh 430 milioni.

Mbali ya vifaa ambavyo ni jezi, soksi, mipira, viatu, mabegi, glovu, vizuia ugoko, vibao vya waamuzi, filimbi pamoja na jezi zao, pia Vodacom imetoa fedha kwa ajili ya kuzisadia timu hizo katika maandalizi yao ambapo hutoa Sh 1.6 bilioni kwa robo ya kwanza ambapo makubaliano ni kutoa kwa awamu nne za msimu huu.

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mambo ya nje ya Vodacom, Salum Mwalimu, alisema: "Kwa mfano kuna timu ambazo zimepanda daraja na uwezo wao kiuchumi ni wa chini kuliko baadhi ya timu kubwa ambazo zina uwezo wa kujiendesha hivyo kwa msaada huu tunaotoa tunazitaka timu hizo ambazo ni Ndanda, Stand United na Polisi Moro zilete upinzani mkubwa kama ilivyokuwa kwa Mbeya City ambao walileta changamoto kubwa msimu uliopita."

Akizungumzia ukomo wa udhamini wao ambapo msimu huu ndio mwisho wa kudhamini ligi hiyo kwa mkataba uliopo, Mwalimu alisema tayari wameanza mazungumzo na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) juu ya udhamini mpya.

"Tupo katika mazungumzo na TFF kama tutaweza kuongeza kudhamini ligi ama tutaishia hapa, lakini naamini kila kitu kitakuwa sawa kwani muda wa mazungumzo bado upo," alisema Mwalimu.

Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo, Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Silas Mwakibinga, alisema: "Kwa sasa timu hazitakiwi kuwa na visingizio kila kitu kimefika kwa muda mwafaka na ukizingatia huu ni mwaka wa mwisho wa udhamini wetu na Vodacom, kila kitu kwa ajili ya msimu huu kinakwenda sawa ila uwanja wa Mkwakwani Tanga ndio upo katika hatua ya mwisho ya marekebisho."

Timu husika ni Azam, Yanga, Simba, Mbeya City, Mtibwa Sugar, Kagera Sugar, Coastal Union, Ruvu Shooting, JKT Ruvu, Prisons, Stand United, Mgambo Shooting, Ndanda FC na Polisi Moro.

Chanzo:MwanaSpoti
 
Back
Top Bottom