Vodacom wanataka kunitapeli.

MotoYaMbongo

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2008
Posts
2,146
Reaction score
887
Naombeni ushauri jamani, Vodacom wamefunga laini yangu ina Pesa, nimewapigia customer care wakasema ilisajiliwa usajili wa muda, wakataka namba ya kitambulisho, Jina langu, Tarehe, Mwezi na Mwaka wa kuzaliwa nikawapa, wakasema ndani ya masaa 24 itakuwa tayari yakapita hamna kitu. Nimehangaika nao kwa siku 8 ikiwamo ya leo bado hamna kitu, kila siku naambiwa subiri ndani ya masaa 24, nimekwenda Voda shop Tabora mjini, nikatakiwa vielelezo nikawapa, wakasema tayari wamepeleka idara husika, nikaambiwa ndani ya masaa 24 yakapita hamna kitu. nikarudi tena hali ikawa ileile. Hadi nimechoka Voda wamenichosha kwa kweli. Jamani naombeni ushauri nifanyeje, Hela zangu zimo katika laini hiyo, shughuli zangu zimekwama.
 
Nenda ofisin kwa meneja na chupa ya chai na godoro, mwambie huondoki mpaka kieleweke. PERIOD.
 
Mkuu kama hutajali unaweza taja kiasi cha pesa zilikuwepo katika simu yako? Kiasi tu sio number ya simu...

Katika kitu ambacho ni rahisi kudai haki yako ni kuibiwa kwa pesa katika simu yako ikiwa mikononi kwa kampuni. Naamini kuwa kutakuwa na usimamizi ama mtiririko mbaya wa kusimamia hayo madai uliosababishia wewe dai lako kuchelewa kushughulikiwa. Hata hivo kama ni siku nane kweli Lazima kuna tatizo kubwa kwa line yako.

Linalo nitia wasi wasi ni kuwa unaambiwa line yako ilisajiliwa kwa muda, hio process ya simu kusajiliwa kwa muda ulishapita kwa kampuni ya vodacom labda tena kama imeanza saizi. Pia naomba kujua ni namba gani ulitumia kupiga simu ili uhudumiwe ili nione kama ni maalum kwa customer care ama lah. Ukinijibu haya ninaweza kuwa na mwongozo.

Tukishindwa haya nitaomba uni PM baadhi ya details ambazo nitakuuliza ili nifuatilie hadi kesho saa sita tatizo lako litakuwa limeshughulikiwa. Pole sana.
 
Naombeni basi kama kuna mwenye namba ya Meneja Mkuu wa Vodacom Tanzania, au kanda ya Magharibi aniwekee hapa ili nitoe malalamiko yangu. Niko njia panda.
 
Hivi ku swap line itakuwa ni ufumbuzi hata kama imezuiwa kupiga sim wakati namba ni ile ile?
 
Wapeleke mahakamani ili wapate adabu
 
Omba mungu password ya mpesa yako isifanane na mwaka wako wa kuzaliwa, ikiwa vinafanana hesabu 50/50 kuibiwa mdogo wangu
 
Ulicheki na Branch Manager? if yes kasemaje? kama kakuzingua ulitafuta contact za HQ na kuelezea mtiririko wa story yako? kama bado fanya ivyo ndani ya masaa12 utapata chako. Wanawachukulia poa huko upcountry.
 
kumbe upo tabora!!! ndio maana, wanyamwezi wanawachukulia poa sababu ya upole wenu wa kinafikinafiki! angekuwa mpare...
 
Yani kwa suala la password wamechemka. Hawawezi kujua kamwe. Isipokuwa wananichelewesha mambo yangu. Ikishindikana kabisa naenda mahakamani kuwashtaki,
 
Yani kwa suala la password wamechemka. Hawawezi kujua kamwe. Isipokuwa wananichelewesha mambo yangu. Ikishindikana kabisa naenda mahakamani kuwashtaki,

Huyo dada hapo juu atakua ni kati ya wahusika wakuu kwenye hiyo kampuni ya simu. Swali la msingi, je ulifanya kama alivyo kuelekeza?
 

Hivi ni nani mwenye dhamana ya usalama wa fedha katika mitandao ya mawasiliano? Yaelekea serikali haina habari kabisa na uhalifu unaofanywa na makampuni haya na kwa njia hiyo kutoa mwanya wa wahuni hawa walioko Voda, Airtel na Tigo. Ni vigumu kutomini kwamba serikali yetu ni dhaifu kutokana na vitimbwi vya makampuni haya ambayo huchezea fedha za watu wapendavyo!
Wanakata fedha wapendavyo, wanawazunguusha wanaotaka kuwasiliana nao baada ya kutenda uhalifu kwa kuyaelekeza mawasiliano kwenye kompyuta, wanatoza fedha kwa huduma zisizokamilika na ushenzi kibao! Sasa nimeamini serikali imesheheni mafisadi kwa maana uhalifu wa Airtel, Voda na Tigo usingeshamiri bila ya kukingiwa kifua na serikali hii tuliyoikabidhi majukumu ya kutulinda na mali zetu.
Mwenyewe nilituma pesa fasta na NMB Sh. 70,000/= kwenda na 0763565245 tarehe 30 Novemba 2012 na ATM ilishindwa kuitoa fedha ile. Nilitarjia kurejeshewa bàada ya siku 3 lakini hazijaejeshwa hadi sasa, karibu mwezi mzima licha ya kuripoti Tawi la NMB nililo karibu nalo na kuhakikishiwa kwamba kiasi kile hakikuchukuliwa! Swali ni watanirejeshea na riba kwa muda wote waliohodhi fedha hizo?
 
Yani sitarudia tena kuweka fedha zangu Vodacom M-pesa au kampuni yoyote ya sim.
 
Mawasiliano ya cm mi naona kama c njia nzui kwani wanaweza kufanya na kukudanganya chochote kwakuwa hawakuoni na uwaoni.sasa hebu funga safari nenda makao yao makuu uonane na manager kisha pia akikuzingua nenda mahakamani.
Kwani ukienda direct mahakamani utauliza manager mkuu anataarifa ?
Atasema hana
utakuwa umeshindwa kesi co onana kwanza manager mkuu,ujue msimamo wake
 
nenda dar,ofc kuu.watakusaidia fasta.ikishndikana,mtafte mch mtikila,muuzie kesi awapeleke mahakami
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…