Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,278
Vodacom Tanzania yazidi kujichafua kuhusu kufukuza wafanyakazi wake.
Kampuni ya simu za mkononi Vodacom iko kwenye zoezi kubwa la kupunguza wafanyakazi wake katika kile kinachojulikana kuyumba vibaya kibiashara.
Katika zoezi hilo lilioendeshwa kwa upendeleo mkubwa limeacha majonzi kwa wafanyakazi walioathirika pamoja na familia zao.
Zoezi hilo limegubikwa na utata kutokana na wakuu kadhaa wa Idara kuwaondoa wafanyakazi ambao walikuwa na chuki bunafsi nao huku wakiwaacha wale ambao ni marafiki zao.
Vodacom ilipiga marufuku chama cha wafanyakazi kuanzisha tawi ili madudu yao dhidi ya wafanyakazi yasijulikane.
Katika hatua nyingine kuna taarifa za uhakika kwamba Vodacom imepanga kudhulumu haki za wafanyakazi inaowafukuza.Kwa idadi kubwa ya wafanyakazi waliofukuzwa ni wale wenye uzoefu mkubwa na kampuni hiyo na ambao wameitumikia kampuni hiyo kwa zaidi ya miaka kumi.
Lengo kubwa la kuwaondoa wafanyakazi wa miaka mingi ni kutokana na chuki kadhaa za mameneja wao ambao wamekuwa wakihojiwa bila kuogopa na wazoefu hao.
Mfanyakazi mmoja aliyeko katika orodha ya kufukuzwa amesikika akilaumu wakuu wa kampuni hiyo kwa kutumia majungu na Fitina kuwafukuza wafanyakazi muhimu na wa miaka mingi bila kuzingatia utu na haki.
Baadhi ya wafanyakazi ambao hawajakumbwa na zoezi hilo wamemuomba Rais John Magufuli, Waziri wa Kazi na Ajira pamoja na Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda kuitupia jicho kampuni hiyo kutokana na kutaka kuonyesha zoezi hilo ni sababu ya utawala wa sasa kubana hiyo kampuni ndiyo maana inawaathiri wafanyakazi.
Hiyo inaonekana ni kuijengea chuki serikali huku watawala wa kampuni hiyo wakitaka kukwepa lawama.