Picha kwa hisani ya Michuzi blog (MODs) naomba msaada picha ikae juu ya hii text. Picha inamuaonesha Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa akikabidhi ndoo ya mafuta kwa Mraribu wa vituo vya kusaidia watumiaji wa dawa za kulevya kuachana na matumisi ya dawa hizo Wete Pemba. Msaada umetoka kwa Vodacom, kampuni ambayo iko chini ya Wizara anayoongoza huyu Prof. Makame Mbarawa.
Kwa vyoyote vile Prof huyu anafanya PR huko kwao Pemba kwa maslahi yake ya kiasiasa. Mpaka hapo sio tatizo, ila shida inakuja kwenye uhusiano wake na kampuni ambayo anasimamia. Kama unapitisha bakuli kwa mtu, ni wazi hutakuwa na kauli tena mbele ya huyo anayekusaidia. Tabia ya wanasiasa wetu kuwa omba omba kwenye makampuni inawageuza mateka wa haya makampuni. Leo hii Prof Mbarawa atakuwa na ujasiri wa kuikemea tena Vodacom kama wateja wanalalamika?
Kuna ulazima kabisa wa kuwa na sheria inatakayoondoa huu mwingiliano wa maslahi na kisiasa na makampuni ya biashara au mashirika ya umma.