VodaCom rekebisheni kero hii Kigoma!

NIMIMI

Senior Member
Apr 2, 2011
170
170
Ni takribani wiki ya nne sasa tangu kusuasua kwa mtandao wa VODACoM na mara nyingine hakuna mawasiliano kabisa.

Wiki mbili zilizopita nilibahatika kuwapata kwa kuwapigia namba yao ya Huduma kwa wateja nikawaeleza kwamba mtandao wa vodaCoM huku Kigoma na wilaya zake ni Kero. Niliulizwa ni kwa simu yangu tu? Nikawaeleza kwa mkoa mzima hasa pale unapojaribu kupiga simu hazitoki majibu ya 'error in connection' kutwa nikajibiwa watalipeleka tatizo kwa wahusika.

Nachelea kusema yalikuwa ni majibu ya kuniondoa kwenye laini kwani hadi ninapo-post kero hii bado mtandao huu ni tatizo kwa mkoa wa kigoma tunakosa huduma za M-PESA hata kuwasiliana.

Je, kwanini msiiondoe Minara yenu kuthibitisha mmeshindwa kuiendesha na kutoa huduma bora kwa wateja wenu?

'THE LEADING NETWORK In Tz' kwa huduma zipi? Wahusika, hili ni Tatizo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom