Vodacom Premier League ' VPL' Simba SC dhidi ya Ndanda FC Uwanja wa Taifa, Kulitaka Mwana!

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Hello Hello.....

Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Vodacom Premier League kuendelea kuvurumishwa leo December 31, 2019 kunako Uwanja wa Taifa, ambapo Mabingwa wa Nchi Simba SC Mnyama Mkali Mwituni, wanawakabili Ndanda FC Wanakuchele kutoka mkoani Mtwara.

Mchezo wa leo unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kwa muda wote wa dakika 90 huku kila timu ikihitaji alama tatu muhimu.

Simba SC, ambayo inaongoza ligi kwa kukusanya alama 31 kwa michezo 12 inahitaji ushindi ili iendelee kujikita zaidi kwenye msimamo wa VPL na kuongeza morali kuelekea mpambano wake na Mtani wake Jumamosi ya January 4, 2020.

Ndanda FC kwa upande wao wanahitaji ushindi mno baada ya msimu huu kuanza kwa kuchechemea, ambapo mpaka sasa ni ya pili kutoka chini ya msimamo wa VPL kwa alama 7 wakiwa wamecheza michezo 13.

Wanasimba na madau wa soka popote ulipo sikiliza matangazo au shuhudia kandanda ya viwango wa shirikisho la soka barani Afrika kutoka kwa Simba SC, Mnyama Mkali kuanzia saa 10:00 jioni..! Usikose Ukaambiwa

Kulitaka Mwana..Kulipewa Mwana

tapatalk_1577790301316.jpeg
IMG_20191231_140325_092.jpeg


••••••••••========•••••

Timu ya Simba SC, leo wameweza kuibuka na ushindi wa mabao mawili bila majibu dhidi ya Ndanda FC kwenye mfululizo wa VPL

Simba walianza kufunga bao la kwanza kwa free kick iliyopigwa na Francis Kahata katika dakika ya 13 ya mchezo.

Deo Kanda aliyeingia baada ya Kahata, aliweza kuhitimisha ushindi kwa kufunga bao la pili kunako dakika ya 85' ya mchezo, kwa matokeo hayo Simba SC wameendelea kujikita kileleni kwa jumla ya alama 34 kwa michezo 13.

FT: Simba SC 2-0 Ndanda FC
 
Kila la heri Mnyama tuupe mkono wa kwaheri mwaka 2019 kwa show ya hatari ya Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana hapo Taifa..SimbaNguvuMoja
 
Kikosi cha kutuliza wadudu warukao na kutambaa, ndani moto nje ndo usiseme..NguvuMoja
 
Kikosi cha Simba kikipasha misuli tayari kwa mpambano wa Vpl
FB_IMG_1577796681404.jpeg
 
Wakati wowote mtanage utaanza Uwanja wa Taifa.

•••Naaaaaaam mpira umeanza ligi kuu Tanzania Simba SC dhidi ya Ndanda FC

00' Simba SC 0-0 Ndanda FC
 
05' mpira unachezwa zaidi eneo la Ndanda FC ambapo mpira wa kichwa wa John Bocco almanusura aandike bao
 
10' Ni free kick kuelekea Ndanda FC baada ya Shiboub kuchezewa vibaya

Anakwendaaaa Kahataaaaaaaaaaa

Goooooooooooooooooooaaal gooooal

Francis Kahata anawatanguliza Simba bao la kwanza kwa faulo iliyoenda moja kwa moja lango la Ndanda FC

Simba SC 1-0 Ndanda FC
 
17' Ajibuuu anakwenda anapigaaaa golikipa Ally Mustafa anapangua na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda
 
Back
Top Bottom