Kwa kweli hata mimi nimeibiwa mno kwa njia hiyo kila ukiweka 1000 wanasema salio halitoshi au huwezi kujiunga salio halitoshi.Voda acheni wiziiiii!
mkuu mimi washaniibiaaa vya kutoshaa yaani nna gazabu nao sana yaani wamenifanya mm boya alafu mimi mteja wa voda kitambo lakini kwa ushenzi huu wanaotufanyiaaa its to much
acheni ushamba bhana smart phone yenyewe tu inakula salio hakikisha kama huna salio basi data iwe off lasivu mtahisi mnaibiwa
piga Vodacom huduma kwa wateje 100 uongee nao watakusaidia watakuambia jinsi waliyokata pesa zako zote kama walikata kimakosa watakurudishia.
Naunga hoja bila hofu yoyote ile hawa voda ni wezi balaa tena usidhubutu kuweka salio la buku alafu ukajiunga kifurushi cha 495 lile salio lilobaki wanalila bila huruma halafu ukiwapigia na kuwafokea wanakujibu "saa hizi unajazba kata simu upige baadae" hii inauma sana
tatizo ni smartphones Unatakiwa unapojiunga hakikisha data Iko off
Habari zenu wana jf,
Ningependa ku-share maumivu ambayo huwa nakutana nayo mara kwa mara pindi niwekapo vocha katika mtandao wa simu wa vodacom.
Leo nmeweka sh 1000 nkajiunga naona ikarudi msg ya kusema salio lake halitoshi eh nkaweka tena 1000 hivyo hivyo maana nilikuwa najiunga kifurushi cha siku.
Cha kushangaza sijapata msg ya mimi kuunganishwa,nikanunua tena 1000 nkajiunga ya siku ikakata nkajiunga tena ya siku ndiyo nkapata mb 150.
Nauliza hivi hela zangu za mwanzo zimekwenda wapi alafu kuna muda mtandao ulisumbua sana au ndiyo walikuwa wanatuibia?
Vodacom acheni wizi, kweli nmeamini lile tangazo lenu la kazi ni kwako limekuwa shida.
tatizo ni smartphones Unatakiwa unapojiunga hakikisha data Iko off
juzi nimeweka 5000 nika jaribu kujiunga kifurushi cha wiki. nikasubiria kama dakika moja hivi message ya kujulishwa kama nimeunganishwa. baada ya kuona kimya nikasema nicheki salio, daaa, empty...leo nimeenda vodashop wananiambia eti whatsapp imekula ela yote hiyo...nimewaachia line yao hapo hapo...AIRTEL sasa hivi mpango mzima.