wiseboy.
JF-Expert Member
- Aug 11, 2014
- 2,931
- 4,549
Kwa kweli siwezi kuvumilia kwa hili,huu ni wizi wa kishenzi kabisa mnataka kunifanya na naapa nitawadhalilisha nyie watu na mtanilipa fidia kubwa sana,leo nimehamisha salio kidogo la pesa kutoka ktk akaunti yangu ya CRDB kwenda m pesa,nipo mbali na benk nikaona huduma hii itanifaa na nina shida hasa sina hata cent,cha ajabu tangu asubuhi hadi sasa pesa haijaingia kwenye m pesa yangu pamoja na CRDB kunitumia msg ya ref kuonyesha kuwa pesa imetumwa ktk m pesa na namba ya ref ninayo,kwenye akaunt yangu nimeangalia salio nikaona limepungua kwa kuhamishwa kwenda m pesa,sasa pesa zangu mmepeleka wapi nyie watu?
Mbona mnaonekana kabisa kuwa mmeniibia,nitawapeleka mahakamani nyote nidai fidia kwa usumbufu mlionipa, nitadai mamilioni ya fidia,mnajitangaza kwa gharama kubwa,kumbe hamna lolote utapeli tu umewajaa,mi nina shida bwana,pesa zangu ziko wapi? tangu asubuhi? nyie ni wezi mmepanga kunipiga kimya,nataka pesa zangu bwana mbona hamna hata aibu nyie mkoje lakini? NATAKA PESA ZANGU MIE NINA SHIDA HAPA NILIPO.
UPDATES

Wakuu,naamini kabisa humu ndani kuna maagent wa vodacom na CRDB,baada ya kuchimba mkwara wa kufa mtu kuwa kwa nini hawajaniwekea pesa zangu tangu asubuhi ambazo nilizihamisha kutoka ktk akaunt yangu kwenda m pesa,nimeshangaa ndani ya dk 30 tu pesa ikawa imeingia,nikajaribu kuhamisha tena laki kwenda m pesa ajabu ndani ya dk 1 tu ikawa imeingia,japokuwa sikutoa details zangu hapa,lakini naamini nimeokoa wengi siku ya leo wasidhulumiwe baada ya maagent wao kusoma mkwara wangu nadhani wali access ili kila aliyefanya transfer apate chake kabla mambo hayajaharibika,hawa jamaa huwa siyo wa kuchekea,ukilemaa wanakuliza kweli,kama ishu ilikuwa mtandao mbona transaction ya pili imechukua dk 1 tu?
wakati kwa kawaida huwa inachukua hata dk 15,acheni wizi wa kishamba nyie,yaani ningewafunga kweli,sasa hivi karoho kametulia,nipo hapa napata safari ya baridi na nimeagiza mbuzi choma kilo nzima,napepesa macho kuona kama naweza kupata ka mrembo kakunifariji night yote hii,usiku mwema wakuu,wacha nile kilaji mtoto wa watu mie