Voda kwa kubadili gia angani hatari sana

ngakotecture

JF-Expert Member
Dec 30, 2014
2,445
2,561
Wakuu wa nchi habari zenu natumai mu wazima,aidha niwape pole kwa shughuri nzito za ujenzi wa taifa letu.Ndugu zangu nina malalamiko kuhusu mtandao wetu pendwa wa vodacom hawa jamaa nawakubali kwa speed yao ya intanet but now nafikiria kuwakimbia kabisaa nisirudi nyuma kwani wamezidi kutunyonya najua sina pa kupeleka malalamiko yangu nikaskizwa ila ni bora nijifariji na wanyonge wenzangu hapa jf cause naweza pata faraja tunatoa pesa nyingi vifurushi vidogo.Kama sasa ivi walikuwa na kifurushi chao cha 1000 unapata 1gb saa 24 jana tu nilipata hizo 1bg kwa buku leo nabonyeza menu yao ya *149*03# nakuta tofauti yani ni gb 10 kwa 10000 na ni wiki mpaka nikachoka nawaarifu nachukua maamuzi magumu naamia halotel jumatatu nasikia mpaka 4g wanayo.
 
Natamani kungekuwa na teknolojia ya kubadilisha line(sim) online
 
Halotel ni wezi, hata kama hupezuri bando linalika kwa kasi kama upo online
Nyie ndo mnaongeza vocha Halotel ukipewa zile MB 30 za kuongeza vocha kwa ubahili wako unaacha kuunga kifurushi eti unakamua hizo 30 mpaka ziishe kwanza matokeo yake unasahau kuunga kifurushi na vihela vyote vinaliwa zile 30 zikiisha. Nimekuelewa vizuri mkuu. Otherwise huku Halotel ni mtelezooooo
 
Kizuri gharama mkuu, kama unataka huduma bora na internet yenye kasi baki Vodacom. Kama unataka unafuu sio ubora nice move.
 
Wakuu wa nchi habari zenu natumai mu wazima,aidha niwape pole kwa shughuri nzito za ujenzi wa taifa letu.Ndugu zangu nina malalamiko kuhusu mtandao wetu pendwa wa vodacom hawa jamaa nawakubali kwa speed yao ya intanet but now nafikiria kuwakimbia kabisaa nisirudi nyuma kwani wamezidi kutunyonya najua sina pa kupeleka malalamiko yangu nikaskizwa ila ni bora nijifariji na wanyonge wenzangu hapa jf cause naweza pata faraja tunatoa pesa nyingi vifurushi vidogo.Kama sasa ivi walikuwa na kifurushi chao cha 1000 unapata 1gb saa 24 jana tu nilipata hizo 1bg kwa buku leo nabonyeza menu yao ya *149*03# nakuta tofauti yani ni gb 10 kwa 10000 na ni wiki mpaka nikachoka nawaarifu nachukua maamuzi magumu naamia halotel jumatatu nasikia mpaka 4g wanayo.
Karibu halotel
 
Nyie mnaolalamika gharama za internet TZ mkienda nchi za watu simu zitakuwa anasa kwenu. Afrika kusini tu wahitaji angalau 25,000/= ili ununue 1GB. Bahati mbaya hao tunaowalalamikia hawauzi internet yao.
 
Wakuu asanteni kwa maoni yenu lakini kinachoniuma mimi kubadili bei za vifurushi pasi na kutupa taarifa yani wanatupeleka peleka tu.
 
Halotel ni wezi, hata kama hupezuri bando linalika kwa kasi kama upo online
Voda ndiyo wezi mara kumi kwanza ukiweka salio tu kabla hata ya kujiunga wao washaanza kukata wajinga sana.......nishatupa line yao.
 
Back
Top Bottom