Vocha za Airtel hazina ubora

Vocha za Airtel hazina ubora

chimpa100

Member
Joined
Mar 28, 2012
Posts
44
Reaction score
5
imekua kawaida sasa hasa kwa mtandao wa airtel kutoa vocha zisizo na ubora pale inapokwanguliwa ipo wap mamlaka husika,wananchi hatujui pakushtaki watu kibao wana vocha za airtel zilizoharibika kwenye wallet zao.Airtel tengenezeni vocha zinazoendana na hali halisi ya kitanzania
 
Ni kweli kabisa hata mimi nimeshapata hasara zaidi ya mara tatu, waliangalie hili ili waongeze ubora.
 
kweli kabisa vocha Airtel ni za kiwango cha chini sana,pamoja na uangalifu bado mara kwa namba zinafutika/kwanguka.Kibaya zaidi inaweza kukuchukua hadi dakika kumi kuwapata customer care,jibu wanalokupa utachoka.Utaambiwa nenda ofisi yao ya karibu au wakala wao.Kwa mzunguko huomtu unajikuta unaachana na hio labda kama ni ya thamani ya juu,imagine watoa huduma wetu walivyo na nyodo then upange foleni kwa ajili ya vocha ya Tsh.500,watakupiga jicho la dharau mpaka ujione hufai wakati ni haki yako.
Wanatakiwa kujirekebishana pia kujaribu kutumia njia mbadala kupunguza mzunguko na usumbufu huu.
 
Its true and very disappointing! The customer care is another head-ache. Baada ya kuona hawana ushirikiano nimeamua kuwapiga ban ya mwezi mmoja kununua vocha zao. Kwani nn bana aakh!
 
Mi nathani wanafahamu ila hawajali pengine wanatarajia kubadili jina,wanakera kwani ukipiga 100 hawapoke/hawapatikani.
 
nilijua peke yangu its true imeshanicost mara kibao mbaya zaidi niko site ambako ni airtel tu inashika kila nikiwapigia wananiambia niende ofisi ya karibu ambayo iko 350km wanatuumiza sana
 
kweli kabisa watu wanahamia ila huduma bado mbovu kwa upande wa vocha wamefeli
 
hii ni kweli kabisa vocha za airtel zinatupa hasara, ukiwapa vocha marejesho zaidi ya wiki.
 
Mimi tangu wanitie hasara sasa hivi nikitaka kurecharge bundle yangu ya Internet nanunuwa kwa kurushiwa sitaki kabisa kusikia mambo ya kukwanguwa.
 
Mimi tangu wanitie hasara sasa hivi nikitaka kurecharge bundle yangu ya Internet nanunuwa kwa kurushiwa sitaki kabisa kusikia mambo ya kukwanguwa.

hapo mkuu ndo suluhisho afu naona pia ndo lengo lao wanasema hawapati faida so wanapromote za kurusha as u know hawa ni oligopoly so walikubaliana waufute vocha za jero ziwe za kurusha ila voda wakaleta zile za 350 asa naona wao wameleta hzi ili tuwetunatumia za kurusha mkuu
 
Back
Top Bottom