Viwavi Jeshi (Armyworms caterpillars) wa aina ya ajabu washambulia mashamba ya Mahindi

Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,943
18,665
Funza au Viwavi wanaojulikana kama Viwavi jeshi ( Armyworms) sasa wamefika Tanzania nakuanza kusambaa kwa kasi. Kwa mara ya kwanza hawa Viwavi Jeshi waligundulika Sauth Afrika. Kwa sasa wameanza kusambaa kwa kasi Africa.

Scientists find crop-destroying caterpillar spreading rapidly in Africa By Reuters

8af19578c23b4eeea91c89a8863f150a.jpg


Kwa sasa wamefika Tanzania na wameharibu mashamba mengi mpaka sasa. Wao wanashambulia mazao ya jamii ya mahindi au Corn. Wanauwezo wa kushambulia hata magugu pale wanapokosa mazao kama mahindi. Wao hawali mazao mengine kama Mbogo mboga na matunda. Wanakula mahindi tu na magugu yanayofanana na mahindi.
4d3d9d94020206730f3048dda2199c49.jpg


Leo nimetembelea mkulima mmoja mwenye shamba la Tikiti. Na kunieleza kuwa Hawa viwavi wapo shamban kwake ila hawali tikiti. Wanakula magugu tena kwa kasi ya ajabu. Waliweza kuzaliana sababu msimu uliopita alikuwa na mahindi shambani kwake ambayo 50% yalitafunywa na hawa viwavi jeshi.

Hawa viwavi Jeshi wanapofika kwenye mahindi hutoa chemical flani ambayo huweza kudanganya mmea kuwa unashambuliwa na magonjwa kama ukungu au fangasi. Pale mmea unapohisi unashambuliwa na hayo magonjwa, hupunguza kinga zidi ya wadudu na kuongeza kinga zidi ya magonjwa. Hivyo huwapa nafasi hawa viwavi kushambulia mmea haraka na kuharibu kwa muda mfupi.

("caterpillar that feeds on corn leaves induces the plant to turn off its defenses against insect predators, allowing the caterpillar to eat more and grow faster, according to chemical ecologists in Penn State's College of Agricultural Sciences.

The finding is one more revelation about the myriad of chemical signals that pass between plants and insects that scientists at Penn State and around the world have been discovering in recent years. In this case, the agent of deceit is the caterpillar's feces, or "frass.")
e607e78d4473769f3f08b12d2a290256.jpg
01cbda83a2be5f6a5af4f22928f05e76.jpg

60354584290c5a41f6a2e961504d906e.jpg



Ushauri.
Wakulima wa mahindi wajitahidi kupiga madawa ya kufukuza wadudu. Kwa sasa haijafahamika dawa maalumu ya kuua hawa viwavi jeshi. Ila nashauri ka sasa kutumia Dasfarm ila haina nguvu ya kumuua huyu mdudu kivile. Inamlewesha tu na wala hafi. Ila husaidia kuwafukuza.

Naendelea na utafiti wa dawa yenye uwezo wa kuuwa hawa funza iliyopo Tanzania kwa sasa. Nikiipata nitaleta Feedback.

Update.

Wakulima wanaweza tumia Majivu kuwafukuza na kuua hwa wadudu. Ila sio efficient sana.
 
kwa kisukuma wanaitwa "Mbilizi/mbilisi..' ni aina ya viwavi hatari sana kwa mazao ya mimea
 
Daaaah hao wadudu no shinda ngoja tutafute dawa tulete feedback Tanzania wataalam wengi tutajua tu
 
Daaaah hao wadudu no shinda ngoja tutafute dawa tulete feedback Tanzania wataalam wengi tutajua tu
Dawa lazima itapatikana maana wdudu wengi kama hawa wanaorginate from laboratory. Na wanaowatengeneza ndyo wanaoleta dawa. Tatizo wataleta dawa baada ya kuwa tumeisha umea ili tuone umuhimu wa dawa yao hata wakiiuza kwa bei ya juu
 
Dawa lazima itapatikana maana wdudu wengi kama hawa wanaorginate from laboratory. Na wanaowatengeneza ndyo wanaoleta dawa. Tatizo wataleta dawa baada ya kuwa tumeisha umea ili tuone umuhimu wa dawa yao hata wakiiuza kwa bei ya juu
Wazungu watu wabaya sana kila jaribio lianzie Africa. Watakuja na dawa ya kuua wadudu ambayo itakuwa na madhara kwa mwanadamu. Hili zoezi la kutafuta dawa tusisubiri wazungu hawa watu watatumaliza. Just saying!
 
Back
Top Bottom