Jamani, hivi kweli hakuna njia mbadala ya kulishughulikia hili jambo?. Kama Lema yuko ndani kwanini tusiache sheria ifuate mkondo wake?, huo mkutano hapo NMC utasaidia vipi katika kutatua tatizo hili?. Kweli imeshindikana kukaa mezani na kulizungumza suala hili kistaarabu?.
Inawezekana kabisa kuna mambo hayaendi ipasavyo lakini pia jinsi ya kudai haki isitumike fujo, busara na hekima itumike badala yake.
Busara hiyo hiyo ingetumika kumwachia Lema hata bila dhamana kwan Lema siyo mtu ambaye unaweza kumtafuta usimpate' wangemtoa ili kuepuka haya yote!