Viwanja vya NMC Arusha: Dr. Slaa akamatwa, Polisi yajaribu kuwaondoa kwa nguvu CHADEMA

LiverpoolFC

JF-Expert Member
Apr 12, 2011
11,348
3,219
Katika kile kilichosadikiwa tangu awali hakika imetimia kwani yapata majira ya saa tisa na nusu hata kumi kasorobo alfajiri,Askari wakiwa tayari kupambana na NGUVU ya UMMA iliyokuwa kwenye mkesha,walivamia uwanja wa NMC na kuwatawanya raia waliokuwa uwanjani usiku kucha kwenye mkesha. Sijajua kama wamejeruhi ama wameua lakini hakika risasi ya moto zilisikika kila corner hp A town.

NAWASILISHA!!


Dr Slaa, nae anashikiliwa Kituoni
 
Ni saa kumi na nusu alfajiri. Mabomu ghafla yanaanza kurindima kwenye viwanja vya NMC Arusha. Tutarajie injuries kwan hadi saa kumi na moja vishindo vya milipuko vinaendelea.
Wanachama wa Chadema walikuwa wamefanikiwa kukesha hadi muda huo na usiku ulipambwa na hotuba mbali-mbali pamoja na nyimbo.
Will keep you posted on new developments
 
Hatua ya Jeshi la Polisi kupiga mabomu muda huu wa saa 11 asubuhi na kuanza kuwatanya wana chadema ni kosa kubwa la ki ufundi, ambalo hawata kaa walisahau.

Maana tayari watu wote wamepanga kwenda NMC asubuhi na hata wale walio lala majumbani mwao wanajipanga leo kuacha sughuli zote na kuingia mjini kwa kasi ya ajabu kuongeza nguvu kubwa ya UMMA ambao wamekesha uwanjani

Kwa maana hiyo basi huyo aliyewashauri kuanza kurusha mamabomu mida hii atajutia uamuzi wake maana tayari watu akili zao wameshajipanga na walitarajia chochote chaweza kutokea kutokana na tabia ya mabavu ya serikali namna ya ku handle mambo hivyo haitakuwa rahisi kwa jeshi la polisi kuwatawanya bila kuleta madhara makubwa kama mwanzo kwa sababu hata watu wengine wamekuja kutoka mikoa ya jirani Kuja kuongeza nguvu kubwa iliyokesha uwanjani hapo.
 
Hali inayoendelea katika jiji la Arusha ni ya kutisha baada+ya jesh la polis kuanza kushambulia mkesha wa chadema eneo la Nmc mjini Arusha.
 
Hatua ya kupiga mabomu muda huu wa saa 11 asubuhi na kuanza kuwatanya wana chadema ni kosa kubwa la ki ufundi ambalo hawata kaa walisahau maana tayari watu wote wamepanga kwenda NMC asubuhi na hata wale walio lala majumbani mwao wanajipanga leo kuacha sughuli zote na kuingia mjini kwa kasi ya ajabu hivyo huyo aliwashauri kuanza kurusha mamabomu mida hii atajutia uamuzi wake maana tayari watu akili zao wameshajipannga na haitakuwa kama mwanzo kwa sababu hata watu wengine wamekuja kutoka mikoa ya jirani.
Asee! Mabomu asubuhi yote hii?
 
Shida zenye misingi ya kisiasa Arusha ni shida na ero kubwa kwa Wa-Tanzania wote kwa ujumla wetu hivyo sote tunahusika katika harakati za kutetea UTU NA UBINADAMU kwa kila mmoja wetu.

Mbio ndio hizo uwanjani Arusha na kusambaa kote kwenye miji mbalimbali nchini.
 
bado mvua ni nyingi sana huku arusha, lakini naona pametulia kidogo. Ndio nakaribia nmc
 
I bet by saa sita mchana hapatakua na occupy nini wala nini.
Huu ndo wakati wa slaa na mbowe kuwa frontline ili tuhakikishe uanamapinduzi wao .wakimsweka risasi ya kichwa tutajua kweli ako na uchungu na injii hii,sio waumie watu wa kawaida
 
Shida zenye misingi ya kisiasa Arusha ni shida na ero kubwa kwa Wa-Tanzania wote kwa ujumla wetu hivyo sote tunahusika katika harakati za kutetea UTU NA UBINADAMU kwa kila mmoja wetu.

Mbio ndio hizo uwanjani Arusha na kusambaa kote kwenye miji mbalimbali nchini.

Bundi bundi karibu Tanzania namshukuru Mungu kutuona na kutujalia pamoja.
 
Muda huu Mi nipo hapa post kabisa TCA narudi uwanjani nikajuwe kilichojiri maana jana niling'atuka pale majira ya ngoma saba kasoro na kuna mabest niliwaacha pale na hata mmoja wao simpati hewani na walikugado kweli kweli. Na ndiyo niamua kama na mbaya na ngoja nikajionee sitaki kuambiwa. Updates ntawapa ya LIVE TOKA NMC ktk hali ntakayoikuta.
 
ila ni vizuri serekali wakaelewana na wananchi wake badala ya kutumia nguvu. Arusha itazua balaa mvua ni nyingi sana lakini patatoka vumbi leo
 
Ngoja natinga hapo uwanjani c muda mrefu kuanzia sasa tarajieni mapya.
 
Back
Top Bottom